Mulugo, NW aagiza Mwl. Nduguru aliyekuwa Mkuu wa S/Sekondari Mabibo akamatwe

 

Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo amefanya ziara katika baadhi ya shule za kanda ya Dar es Salaam  na kuagiza aliyekuwa Mkuu wa shule ya sekondari Mabibo, Dominick Ndunguru akamatwe na kulipa shilingi milioni tano fedha zilizotokana na ada za wanafunzi ambazo anadaiwa kutoweka nazo.

Katika ziara hiyo, Mulugo ameshuhudia baadhi ya wanafunzi ambao matokeo ya mitihani yao yamezuiliwa wakiendelea na masomo ya kidato cha tatu ijapokuwa bado hawajui kama wamefaulu au la katika mitihani ya kidato cha pili.

Sakata la baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili kanda ya Dar es Salaam kukumbwa na sintofahamu iwapo wanaingia kidato cha tatu au la kutokana na matokeo yao kuzuiliwa limechukua sura mpya ambapo Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo amefanya ziara katika shule za Sekondari Mabibo, Temeke,Tandika na Azania.

Shule ya kwanza kutembelewa ni Mabibo ambapo wanafunzi wote hawajapata matokeo yao sababu aliyekuwa mkuu wa shule hiyo Dominick Ndunguru kutoweka na fedha za ada.

Kituo cha pili kikawa ni Temeke na hapo wanafunzi wameingia Kidato cha tatu japo hawajui kama wamefaulu au la! Lakini Azania wanafunzi 126 hawajalipa ada ya mitiahani iliyosababisha matokeo yao kuzuiliwa.

Zaidi ya shilingi milioni 126 ambazo ni ada ya Mtihani wa kidato cha Pili bado hazijawasilishwa kwa Mkaguzi wa kanda ya Dar es Salaam.

Upendo Wella, 
TBC, Dar es Salaam

Post a Comment

Previous Post Next Post