SHEREHE ZA KUAGA MWAKA 2012 NA KUAGA WATUMISHI LUDEWA ZAFANA -LIVE


Mkurugenzi  wa Ludewa Fidelis Lumato 

Sherehe za kuwaaga na kuwakaribisha watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa zafana usiku huu katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa . Katika sherehe hizo ambazo pia zimeambatana na kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 zinafanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Ludewa huku viongozi mbali mbali wa Wilaya na Halmashauri hiyo ya wilaya ya Ludewa wakiwa wamepamba sherehe hiyo.

 Akizungumza katika sherehe hiyo mratibu wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Gladness Mwano amesema kuwa katika sherehe hiyo jumla ya watumishi 6 wanaagwa rasmi baada ya kustaafu na watumishi 14 wanahama huku watumishi 5 wakikaribishwa katika Halmashauri hiyo ya wilaya ya Ludewa .

Watumishi wanaostaafu katika Halmashauri hiyo ni pamoja na Augusta Kayombo ( Idara ya afya), Gerold Kayombo ( katibu TSD), Ignas Mkechi (ukaguzi wa shule), Beneth Nzalamoto ( Idara ya afya) , Edwird Masangula (idara ya fedha) na Ireen Mtetemela ( idara ya utawala).


Wakati watumishi waliohama ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Hilda Lauwo aliyehamia Maswa , Juma ,Ally (afisa utumishi na utawala aliyehamia Mbinga, Advery Dallu Afisa utumishi na utawala amehamia TAMISEMI Dodoma, Alto Liwolelu (Mwanasheria aliyehamia Kilolo), Emmanuel Mlelwa (afisa elimu sekondari aliyekwenda Pangani ,Christopher Nyandiga (mhandisi aliyehamia RAS Njombe), Rashid Mtamila ( Mhandisi wa ujenzi aliyehamia Sumbawanga),Gumbo Mvanda ( afisa misitu anahamia Ras Njombe),Daud Kumburu (afisa ufugaji nyuki anahamia Ras Njombe ), Mussa Sechonge (Afisa kilimo wadudu anakwenda Morogoro),Rose Lutambi (muunguzi mifumo ya kompyuta anakwenda Njombe mji) na Mariam Kinyamagoha (afisa muuguzi anahamia Mufindi).

 Aidha Halmashauri ya wilaya ya Ludewa imepokea watumishi wapya ambao wanachukua nafasi ya waliohama na kustaafu ikiwemo nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo inayochukuliwa na Fidelis Lumato aliyehamia kutoka Tarime, Mathan Chalamila (mwanasheria anayehamia kutoka Njombe DC ,Maternus Ndumbaro (afisa elimu sekondari anayehamia kutoka Makete , Baraka Mkuya (mahandisi ujenzi anayehamia kutoka Sumbawanga MC na Antony Mbi
nda (katibu TSD anayehamia kutoka Mufindi)

Akizungumza katika sherehe hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mateo Kongo alisema kuwa Halmashauri hiyo imefarijika kwa utendaji wa watumishi waliopita na kuwakaribisha wapya huku akiahidi kuwapa ushirikiano zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post