TASWIRA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS: MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikipita na kutoa heshima mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Maraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride wakati wa Sherehe za Mapinduzi, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakati alipomaliza kukagua gwaride la  Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza  na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
 Baadhi ya viongozi..jukwaa kuu.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar na Ofisi ya Makamu wa Rais

Post a Comment

Previous Post Next Post