Algeria kwa sasa inashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa timu bora barani Afrika.
Kwa mujibu wa takwimu za FIFA, timu hiyo kwa mara ya kwanza ilikuwa miongoni mwa timu 20 bora zaidi duniani Novemba mwaka uliopita.
Na ikiwa takwimu hizo ni za kuaminika, basi Algeria ina nafasi nzuri ya kushinda mechi yao dhidi ya majirani na mahasimu wao Tunisia.
Kundi D ndilo kundi linalokisiwa kundi ngumu zaidi katika mashindano ya mwaka huu kwa kuwa inajumuisha Ivory Coast, Togo, Tunisia na Algeria.
Hata hivyo Algeria haikufuzu kwa fainali za mwaka uliopita na katika mashindano mengine imeondolewa katika hatua ya kwanza au raundi ya pili.
Lakini kikosi cha mwaka huu, kinaonekana kuwa bora na inajumuisha kipa Rais Mbolihi ambaye amewahi kufanya majaribio na klabu ya Manchester United.
Wachezaji wa Zamani kama vile Karim Ziani, Nadir Belhadj na Antar Yahia waliondolewa kwenye kikosi cha mwisho na mahala pao kuchukuliwa na wachezaji chipukizi kama vile nyota wa Valencia Sofiane Feghouli na Foued Kadir.
Tunisia kwa upande wake inamtegemea mcheza kiungo Youssef Msakni ambaye anajulikana kwa jina la utani kama '' Little Mozart''.
Katika mashindano manane waliyoshiriki Tunsia, ilifika hatua ya robo fainali na endapo kikosi chake kinachojumuisha vijana chipukizi, kitacheza kama ilivyotarajiwa basi, mechi ya kundi hili zitakuwa ngumu sana.
Post a Comment