Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize, REUTERS/Luc Gnago
Na Flora Martin Mwano
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amemvua madaraka
Waziri Mkuu wa serikali yake Faustin Archange Touadera ikiwa ni mojawapo
ya hatua za utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali
na waasi wa Seleka katika mazungumzo ya kusaka amani ya Taifa hilo
yaliyofanyika mjini Libreville nchini Gabon.
Tangazo la kuvuliwa madaraka kwa Waziri Mkuu lilitolewa kupitia radio ya
umma jana jumamosi na nafasi hiyo inatarajiwa kuzibwa na Waasi wa
Seleka ambao wamekubaliana kuunda serikali ya umoja wa Kitaifa na
serikali iliyopo madarakani hivi sasa.
Uamuzi huo umepokelewa kwa furaha na wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati ambao wameathiriwa na mapigano hayo yaliyoambatana na ukikwaji
mkubwa wa haki za binadamu hususani wanawake na watoto.
Vyanzo vya habari toka upande wa upinzani vimedokeza kuwa huenda nafasi
hiyo ikachukuliwa na Mwanasheria Nicolas Tiangaye ambaye aliongoza
ujumbe wa waasi katika mazungumzo ya nchini Gabon, wakati wengine
wakimtaja mwanasheria mwingine Henri Pouzere ambaye naye ameshiriki
katika mchakato huo.
Mazungumzo ya amani yaliyofikia uamuzi huo yandaliwa na Jumuia ya
Kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati yalihudhuriwa na Rais wa Gabon Ali
Bongo, Rais wa Jamuhuri ya Congo Brazaville Denis Assou Nguesso ambaye
pia ni msuluhishi wa Mgogoro huo na Rais wa Chad Idriss Deby Itno ambaye
ni Mshirika wa karibu wa Bozize.
Wanajeshi takribani mia tano kutoka Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo DRC, Chad na Cameroon walipelekwa nchini humo kulinda amani mwaka
2008, na kumekuwa na taarifa kuwa wameanza kuondoka nchini humo.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
Post a Comment