
Meneja
bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akionyesha kipeperushi cha huduma
ya SMS kichizi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo itakayowawezesha
wateja wa Airtel nchini kutuma ujumbe mfupi wa sms kwa shilingi 1 kwa
sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma
Mwapachu kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
Airtel Product Manager Francis Ndikumwami display brochure of new launched service dubbed SMS kichizi that enable Airtel customer to send sms to all network across the country at the cost of 1 shilling 24hours 7 days a week. on the right is Airtel Brand Manager Rahma left is Public Relations Officer Jane Matinde

Meneja bidhaa na masoko Francis Ndikumwami akiongea
na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma ya SMS kichizi ambapo
wateja wa Airtel sasa wanaweza kutuma ujumber mfupi (sms) kwa gharama ya
shilingi 1 kwa sms masaa 24 kwa siku 7 za wiki, katikati ni na kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Rahma Mwapachu
Product
Manager Francis Ndikumwami speaks to the press during the launch of SMS
kichizi sms service that enable Airtel customer to send sms to all
network across the country at the cost of 1 shilling 24hours 7 days a
week. in the picture is Airtel Brand Manager Rahma Mwapachu (right) and
Public Relations Officer Jane Matinde (left)
Wateja wa Airtel sasa kutuma SMS kwa Shilingi Moja
· Ujumbe mfupi utatozwa shilingi 1 badala ya shilingi 54 kwa sms
· Sms kwenda mtandao wowote nchini
3 January 2013, Airtel
Tanzania kampuni ya simu inayoongoza kwa mtandao mpana na huduma bora
na bei nafuu leo imetangaza bei mpya yenye punguzo la gharama za kutuma
ujumbe mfupi ili kuwapati wateja wake urahisi na unafuu wa huduma ya
ujumbe mfupi nchini. Airtel imepunguza gharama za sms kutoka shilingi
54 hadi shilingi 1 kwa kila sms.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa gharama mpya ya sms Meneja bidhaa na masoko
Francis Ndikumwami alisema” Leo tunayofuraha kuzindua SmS Kichizi ofa ya peeke itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu.
hii ni ya kwanza kutoka Airtel ambapo tumewapatia na kuwawezesha wateja
wetu nchi nzima kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa gharama nafuu ya shilling
1 kwa kila ujumbe mfupi kwenda kwenye mtandao wowote masaa 27 siku 7 za
wiki bila kikomo. sasa wateja wa Airtel watatozwa shilling 125 kwa
ujumbe wa kwanza wa sms na zingine zitakazofuata zitatozwa gharama ya
shilling moja kwa siku”.
“SMS
kichizi huduma ya ujumbe mfupi ni mwendelezo wa kutimiza dhamira yetu
ya kutoa huduma bora, kuwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma
zetu za wateja na kutoza gharama nafuu. Airtel leo ndio mtandao ulioenea
zaidi maeneo mengi nchini na kuwafikia watanzania wengi zaidi kupitia
huduma zetu za Airtel money na internet yenye kasi zaidi nchini.”
aliongeza Ndikumwami
Gharama
hizi mpya za ujumbe mfupi zitatozwa kwenda mitandao ya ndani ya nchini
tu na ni kwa wateja wa Airtel wa malipo ya awali nchini.
Akiongea
kuhusu muda wa huduma hii Francis Ndikumwami alieleza, Airtel
tunawajali wateja wetu hivyo huduma hii ya SMS Kichizi sio promosheni ni
huduma ya kudumu.
Airtel
bado inaendelea na promosheni yake ya msimu wa sikukuu ya Amka
millionea ambapo wateja wengi nchini nzima wameendelea kujishindia pesa
taslimu ambapo wateja zaidi ya 300 wameshajishindia jumla ya pesa
taslimu zaidi ya shilling million 120 hadi sasa.
Post a Comment