MOJA YA MTOTO MAJERUHI AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISION CHIMARA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MOJA YA MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU
HILI NDILO ROLI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA KAPUNGA
KWELI MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA POLE MMOJA YA WATOTO WALIOPATA AJALI
HUYU BINTI NI MWANAFUNZI NAE ALIKUWEPO KWENYE AJALI HIYO
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
HAWA WOTE NI WANAFUNZI WALIKUWA WANAENDA KUFANYA KIBARUA CHA KULIMA KWA MWEKEZAJI KATIKA SHAMBA HILO LA KAPUNGA
MAJERUHI 22 WAKIPAKIZWA KATIKA ROLI AINA YA FUSO TAYARI KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MAJERUHI WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA
MWANDISHI WETU JOSEPH MWAISANGO AKITOKA KATIKA HOSPITALI YA CHIMALA
BAADA YA KUSHUHUDIA NA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA MAANA TAARIFA YA AWALI
ILITOLEWA KUWA WATU WASIOZIDI 30 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI SASA
TUNAHABARI KAMILI BAADA YA MBEYA YETU KUFIKA KATIKA TUKIO
WATU watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku
hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani
kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Mapogolo kata ya Itamboleo
Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali
ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao
walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba
vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha Kapunga.
Lori hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa
likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli, lilionekana
likiwa katika mwendo kasi na dereva huyo akiwa na lengo la kutaka
kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao
ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya
majeruhi alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari
hilo na kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye
aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata
taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam
Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa madaktari,
kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu kwa
ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya
kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na
mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa
Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde
Mbeya Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika ajali hiyo
kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto
waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.
Picha Mbeya yetu na Kamanga
Post a Comment