Mabingwa
wa mapinduzi cup Azam fc leo wameanza na ushindi katika michuano ya
kombe la shirikisho (CAF Confideration cup) baada ya kuwachapa goli 3-1
Al-Nasri JUba mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Azam fc kama ada yao kuhakikisha kupata goli katika dakika ya
20 ambapo dakika ya 14 Abdi Kassim Babi aliifungi. azam fc goli la
kuongoza akiunga mpira wa Kipre Tchetche.
Baada ya goli hilo
kuingia azam waliendelea kulisakama lango la al-nasri na katika dakika
ya 16 Brian Umonyi alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na
nafasi yake kuchukuliwa na Khamis Mcha.
Katika dakika ya 28
Michael Bolou aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Jabir Azizi. na
katika dakika ya 38 al-nasri wal4rwawazisha goli hilo kupitia kwa Fabian
Alies na kupelekea timu kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.
Kipindi
cha pili azam waliuwanza mchezo kwa kasi na kupoteza nafasi kazaa
kupitia kwa Abdi Kasim na katika dakika ya 62 Abdi Kasim alienda benchi
na nafasi yake kujazwa na John Bocco ambaye aliingia kwa kasi na kukosa
nafasi ya goli.
Katika dakika ya 79 Kipre Herman Tchetche
aliandika goli la pili kwa azam fc akimalizia kwa kichwa kazi nzuri ya
Khamisi Mcha Viali goli lilizidisha hamasa kwa azam ya kusaka goli 3.
Alikuwa
Kipre Herman Tchetche aliyehitimisha kalamu ya magoli kwa kuifungia
goli la 3 azam fc katika dakika ya 90 na kupelekea mchezo kumalizika kwa
azam kushinda goli 3-1.
Azam fc leo wangetoka na magoli memgi
kama sio uhodari wa kipa wa al-masri aliyeokoa michomo lukuki toka kwa
washambuliaji wa azam.
Azam na al nasri watarejeani kati ya machi 1-3 katika mji wa Juba Sudan kusini.
azam
leo; MWADINI ALLY, HIMID MAO, MALIKA NDEULE, DAVID, JOACKINS ATUDO,
MICHAEL BOLOU/JABIR AZIZI, SALUM ABOUBAKARY, HAMPHREY MIENO, ABDI KASIM /
JOHN BOCCO, BRIAN UMONY /JHAMISI MCHA, KIPRE TCHETCHE
Post a Comment