Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza katika kiwanda cha bia cha Serengeti, ambapo amesema kutokana
na hali alioiona pale, itabidi kwanza kuwashirikisha NEMC na kuona
jinsi gani watashauriana na kama itabidi kukifunga itabidi aondoe hati
ya mazingira kisha kukifunga kiwanda hicho.
Na.Mo Blog Team.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza leo
ameendelea kufanya ziara za kushtukiza katika viwanda na mahoteli
mbalimbali jijini Dar es salaam kuangalia hali ya usafi wa mazingira.
Katika
ziara hiyo Mh waziri na ujumbe wake wametembelea kiwanda cha Bia cha
Serengeti, CI Group Marketing Solution, Coco Beach, hoteli za Golden
Tulip na Sea Cliff.
Akitoa
maamuzi kuhusu mazingira aliyoyakuta katika kila sehemu, Mh. Dkt.
Huviza amesema Kiwanda cha Serengeti kina mfereji unaomwaga maji machafu
na bahati mbaya unatitirisha katika makazi ya watu kitu ambacho ni
hatari, hivyo atashauriana na NEMC na Mwanasheria waone jinsi ya
kuwasaidia, lakini kama itashindikana kwa kuwa maji wanayomwaga ni mengi
sana itabidi wafunge kwa muda.
Kuhusu
maeneo mengine aliyoyatembelea Mh. Waziri amesema hawezi kutoa maamuzi
kwa sasa kwa sababu kila aliyekutwa na makosa amepewa muda wa
kuyarekebisha na ambaye atashindwa kufanya hivyo basi atafungiwa kwa
mujibu wa sheria.

Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa
akiwasili katika kiwanda cha bia cha Serengeti Breweries baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda hicho kujionea namna gani
wanatunza Mazingira.


Afisa
Mazingira wa Kiwanda cha Serengeti Breweries Dominick Elibariki akitoa
maelezo ya namna wanavyotibu maji taka ya kiwanda hicho kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza
aliyeambatana na maafisa kutoka Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC).

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huviza
akiendelea na ukaguzi wa maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho.

Moja
ya mtaro unaotiririsha maji yenye kemikali yanayotoka ndani ya kiwanda
cha Kampuni ya Serengeti Breweries uliolekezwa na kupitisha maji yake
yenye harufu kali karibu na makazi ya watu.

Sehemu
ya mtaro wa maji machafu yanayotoka ndani ya kiwanda cha bia cha
Serengeti ambao umesafishwa na kulundika lundo la uchafu pembezoni mwa
ukuta wa nyumba ambayo ni makazi ya watu.

Mkazi
wa Kata ya Chamwenyewe iliyopo maeneo ya Chang’ombe Bi. Mwaka Washokera
akimweleza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt
Terezya Huvisa adha anayoipata yeye na familia yake kutokana na mtaro wa
maji machafu ya kampuni ya bia ya Serengeti ambao umepita uwani kwake,
na kipindi cha mvua kusababisha maji machafu yenye kemikali kuingia
katika nyumba yake.
Mama
huyo pia amesema kampuni hiyo imemnyanyasa kijinsia kwani alikuwa
akilima bustani ya Mboga uwani kwake lakini kutokana na mtaro huo kupita
karibu na uani kwake ameshindwa kuendelea na bustani hiyo amelalamikia
pamoja na moshi mzito unaotoka ndani ya kiwanda hicho na kusababisha
watoto kukohoa kila mara.

Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mh. Dkt Terezya Huvisa
akiangalia mtaro wa maji machafu uliopita uani kwenye nyumba ya Mama
Mwaka Washokera.

Afisa
Mkuu wa Mazingira wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) Bi. Ruth Lugwisha akichukua sampo ya maji
yanayotiririka kutoka katika kiwanda cha Serengeti Breweries kwa ajili
ya vipimo kama yana madhara kwa binadamu ambapo bomba lake limeelekezwa
kwenye makazi ya watu.

Mtaro
wa maji yenye kemikali unaotokea kwenye kiwanda cha CI Group cha
uchapishaji kilichopo jirani na kiwanda cha bia cha Serengeti kilichopo
maeneo ya Chang’ombe.

Mkazi
wa Kata ya Chamwenyewe Bi. Mwamtema akimuonyesha Waziri wa Mazingira
Dkt. Therezya Huvisa adha wanayoipata kutokana na maji yanayotiririka
kutoka kwenye viwanda hivyo ambayo hujaa katika mifereji hiyo na kuingia
katika makazi.

Mmoja
wa wafanyakazi wa kiwanda cha CI Group akimuonyesha Waziri Upande
zilipo Ofisi za mabosi wa kampuni hiyo ambapo katika Mazingira ya
kutatanisha walikuwa hawaonekani kiwanda hapo baada ya Waziri kuingia
lakini cha kushangaza magari yao yalikuwa yamepaki nje ya ofisi hizo
kuonyesha kwamba wapo ndani.

Pichani
Juu na Chini ni sehemu ya kupunguza stress wanayotumia wafanyakazi wa
kiwanda cha CI Group wakiwa wameandika ujumbe unaosemeka” Tumechoka na
Vyoo” ambapo Mheshimiwa Waziri aliamua kuingia kukikagua na kujionea
hali halisi.

Kumradhi kama picha hii itakukwaza lakini haya ndio mazingira ya kazi kwenye baadhi ya viwanda vyetu nchini.


Baadhi
ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakifurahia ujio wa Waziri wa Mazingira
wakijua ya kwamba wataboreshewa mazingira ya kufanyia kazi.

Pichani Juu na Chini Waziri wa Mazingira Dkt. Therezya Huvisa akikagua mtaro wa maji machafu ya kiwanda hicho.

More Pictures http://dewjiblog.com/

Post a Comment