BARAZA LA HABARI TANZANIA LIMEWAAPISHA MAJAJI

Baraza la habari Tanzania limewaapisha majaji watakao simamia tuzo za umahiri wa uandishi wa Habari kwa mwaka 2012,ambapo limewataka Majaji hao kuhakikisha wanatenda haki na kuchagua kazi zenye ubora unaotakiwa, ili kutoa hamasa zaidi kwa Waandishi katika tuzo zijazo pamoja na kuinua kiwango cha Uandishi wa Habari nchini.
Akizungumza mara baada ya kumaliza jukumu la kuwaapisha majaji hao Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya MCT, Jaji Mstaafu THOMAS MIHAYO amesema kazi ya msingi ya majaji hao ni kuteua kazi zitakazoonekana kuwa na maslahi kwa Taifa, hivyo majaji hao wanapaswa kufanya kazi hiyo kwa kimisingi ya kizalendo na kuepuka kupendelea chombo chochote cha Habari.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa MCT KAJUBI MUKAJANGA, ametaja makundi pamoja na mikoa iliyoleta kazi nyingi zaidi katika Tuzo za Mwaka huu, ambapo zaidi ya kazi 900 zimewasilishwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post