MZUNGUKO wa
pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu zaidi kwa jina la Grand Malt
Premier League, unatarajiwa kuanza leo pale kutakapokuwa na michezo
miwili kati ya Mafunzo na KMKM zitakazokwaana katika Uwanja wa Amaan, huku Chipukizi na Falcon wakionyeshana kazi ndani ya Gombani, Pemba KMKM
miwili kati ya Mafunzo na KMKM zitakazokwaana katika Uwanja wa Amaan, huku Chipukizi na Falcon wakionyeshana kazi ndani ya Gombani, Pemba KMKM
wanaingia uwanjani wakitaka kuendeleza ubabe wao, kwani mpaka sasa ndio
wanaoongoza ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 23, wakati Mafunzo
ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 22.Ugumu
wa mchezo huo ni kuwa kila timu itataka kujiimarisha zaidi kwani
kuteleza ni kujiweka katika mazingira magumu ya kutwaa taji na iwapo
KMKM itakubali kichapo, itaichia Mafunzo kushika usukani wa ligi hiyo
yenye timu 12.
Chipukizi wao watataka kuutumia vema uwanja wa
nyumbani, kwani ikiwa nafasi ya tano kwa pointi 17 ilizonazo itataka
kuhakikisha inashinda, ili kuzidi kupaa katika msimamo wa ligi hiyo
ambayo kwa sasa imeongezeka mvuto kutokana na udhamini wa Grand Malt. Lakini
wasitegemee mteremko kutokana na Falcon nayo kutaka kujinasua kutoka
nafasi za chini. Kwa sasa timu hiyo inashikilia nafasi ya tisa ikiwa na
pointi 13. Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho, pale kutakapokuwa na michezo miwili wakati
Bandari na Malindi zitakapokwaana Uwanja wa Mao, huku Jamhuri na Duma
zikionyeshana ubabe Uwanja wa Gombani, Pemba na Jumapili kutakuwa
na mchezo mmoja tu kati ya Zimamoto na Mtende zitakazocheza ndani ya Mao.
Timu inayoshika mkia mpaka sasa ni Mundu ikifuatiwa na Malindi. Timu zote hizi zina pointi saba kila moja. Mchezaji
anayeongoza kwa kupachika mabao ni Ali Manzi wa Mtende mwenye mabao
saba, akifuatiwa na Faki Mwalimu (Chipukizi) na Juma Mohamed (Chuoni)
walio na magoli sita. Ligi Kuu ya Zanzibar kwa sasa inadhaminiwa na
kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt
Post a Comment