
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akivuta waya kuashiria kufyatua mtego wa kuwasha moto wa kuteketeza
Silaha haramu, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo la
uteketezaji wa silaha haramu, Lililofanyika katika Kambi ya Magereza
jijini Dar es Salaam, Jumamosi Feb 16, 2013. Kushoto kwake ni Kamishna
msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Siro na wa pili kulia kwake
ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perera Ame Silima na Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kmataifa, Benard Membe.

Sehemu
ya Silaha hizo zikianza kuteketea kwa moto baada ya Makamu wa Rais,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufyatua waya maalumu wa kuwasha moto huo.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, baada ya kusimamia
zaoezi la uteketezaji wa Silaha haramu, lililofanyika Ukonga jijini Dar
es Salaam.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, wakati
wakipita kukagua sihala hizo haramu kabla ya kuanza kwa zoezi la
uteketezaji wa silaha hizo haramu lililofanyika Ukonga jijini Dar es
Salaam.

Silaha haramu zilizoteketezwa.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha Haramu,
lililofanyika Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.
-
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
ameongoza zoezi la uteketezaji silaha haramu na kuwataka wananchi
kushirikiana na serikali katika kuwafichua wanaomiliki silaha hizo
mapema kabla athari haijawa kubwa zaidi.
Akizungumza
katika zoezi hilo la kuteketeza silaha haramu, ambalo limefanyika
pamoja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye viwanja
vya Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema kila
mwananchi ni mlinzi wa kwanza wa amani ya nchi yake na wanaomiliki
silaha haramu ni wazi kuwa siyo raia wenye malengo mema na amani ya nchi
zao.
Post a Comment