Mke Wangu Amwajiri House Girl Ambae ni Changudoa Nilie Wahi Tembea Naye Kona Bar

Tukio hili lilinitokea siku nyingi kiasi, kama miaka kumi iliyopita, lakini nalikumbuka hadi leo kwa sababu liliniletea balaa kubwa na kuhatarisha ndoa yangu kuvunjika ambayo bado ilikuwa changa. Hivi sasa nakubaliana na ile methali isemayo, za mwizi ni arobaini. Nakumbuka wakati huo nilikuwa nakunywa mbili-tatu hivi na kidogo nilikuwa napenda wanawake. Lakini wanawake zangu walikuwa ni wale ambao hawana gharama kubwa na ambao mkishamaliza mambo yenu basi.

Nilikuwa najiamini sana wakati huo kuwa kamwe sitofumaniwa kwa sababu wanawake wenyewe walikuwa ni wale wanaojiuza na kwao walikuwa hawahitaji kujua jina wala namba ya simu na pia hawakuwa na wivu hata uwabadilishe kila siku. Nilikuwa nawachukua kwa ule mtindo wa cash and carry, na walikuwa wananipenda kwa sababu nilikuwa siombi kupunguziwa bei sana sana nilikuwa nawaachia keep chenji, yaani kama nimewapa hela kubwa sidai chenji yangu.

Kiwanja changu kikubwa kilikuwa ni pale Africa Sana katika baa Maarufu iitwayo Kona Bar. Nilikuwa nakipenda sana kile kiwanja kwa sababu kilikuwa na totoz za kufa mtu, ilikuwa kila siku unakutana na kipusa kipya mpaka unashangaa miujiza ya mwnyezi Mungu na bei zao zilikuwa affordable kabisa kulingana na kipato changu.

Wakati huo nilikuwa nimejidanganya kwamba, isingekuwa rahisi kufumaniwa na kahaba na ndoa yangu ilikuwa na amani wakati wote. Tofauti na mabinti wa siku hizi ukiwatongoza tu, subiri hizo meseji za usiku wa manane na missing call za mida ya hatari, hapo bado hujaletewa bili ya matumizi ya saloon na makochokocho mengine ambayo hata mkeo hujawahi kumnunulia.

Niliwapenda sana wale makahaba wa Kona Bar kutokana na utaratibu wao wa cash and carry. Mara kadhaa angalau mara moja kwa wiki nilikuwa natembelea eneo hilo la Kona Bar na kujitwalia mrembo wa kwenda kujivinjari naye kwa masaa kadhaa kabla ya kurudi nyumbani. Kwa kuwa kazi zangu zilikuwa hazina ratiba maalum , ilikuwa ni sababu nzuri ya kutenda uovu wangu. Uzuri wa Baa ile ulikuwa ni mmoja, yaani kila siku lazima ukutane na kipusa kipya, leo unamkuta huyu, kesho yule na keshokuta mwingine, mpaka unashangaa kwamba huwa wanatoka wapi.

Tabia hiyo niliendelea nayo kwa muda wa miaka miwili hivi, kabla ya kuiacha. Kwa nini niliiacha? Tega sikio.

Siku moja niliwasili nyumbani jioni nikitokea kazini kwangu. Wakati huo tulikuwa na tatizo la msichana wa kazi wa kutusaidia pale nyumbani yaani hausigeli kama wanavyoitwa. Kwa wiki mbili mke wangu alikuwa anahangaika kutafuta msichana wa kazi. Nilipofika nyumbani jioni hiyo, mke wangu alinifahamisha kwamba, alikuwa amepata binti wa kazi. Nilifurahi sana kusikia hivyo na nilimuuliza alipo. Mke wangu alisema huyo binti anaoga. Niliuliza kama ni mkubwa au ni mdogo sana. Mke wangu alinijibu kwamba, ni mkubwa kiasi, msichana wa makamu.

Kwa hiyo baada ya kuoga, huyo msichana aliambiwa na mke wangu aje sebuleni ili atambulishwe kwangu na nizungumze naye kwa ajili ya kumfanyia tathmini.

Alikuja sebuleni. Alipokanyaga tu sebuleni, moyo wangu ulifanya dat…! Hata yule binti alisita na mke wangu alimwambia asiogope. Mke wangu alijua yule msichana alikuwa amesita kwa kuogopa, kumbe wala. Alinisalimia kwa shikamoo dhaifuuuu…..sana. Niliitikia na nilikuwa natetemeka kidogo. Mke wangu alimtambulisha yule hausigeli kwangu. Halafu alituacha tuzungumze.

‘Umefuata nini hapa, yaani sasa unajifanya wewe hausigeli, changudoa. Yaani unadhani nitakuruhusu ufanye kazi hapa uniharibie watoto.’ Nilianza kwa kumtisha Yule msichana.
Unafikiri ni kwa nini?

Katika ile okota okota yangu kule Kona Bar, huyu msichana naye nilishamchukua mara kadhaa na alikuwa akiniona nikiondoka na machangudoa wengine katika eneo hilo mara kwa mara.

Yule msichana alicheka baada ya mimi kusema maneno yale. Halafu aliniambia, ‘naomba 50,000/= kama unataka niondoke hapa kwako bia kuharibu.’ Halafu alinyamaza huku akinibenulia midomo kama binti wa kizaramo anayependa kuzodoa wenzake. Hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo. Kweli kuna mijanajike sugu jamani……..

Nilisimama na kwenda chumbani. Halafu haraka nilirudi nikiwa na kitita cha hizo fedha, kwani sikutaka pazuke balaa. Nilimkabidhi haraka yule binti, huku nikamwambia, ‘nenda zako, nitamwambie mke wangu kwamba, nimeona huwezi kazi, haya uondoke sasa hivi….’ Nilimwambia huku nikiwa nimemkazia macho…

Kumbe yale mazungumzo ya awali, mke wangu aliyasikia, na hivyo akaamua kubana karibu na sebule ili kusikiliza kinachoendelea. Alinifuma, wanaita red handed, yaani laivu kabisa.

Ilibidi nieleze ukweli na kwa hali hio nilimnyang’anya yule binti pesa zangu na kumtishia polisi. Aliondoka lakini mtaa mzima pale Tabata Ubaya Ubaya ulijua kila kitu kuhusu balaa ile, maana yule changudoa aliongea kama hana akili timamu. Kuanzia siku hiyo, pombe nikaacha na mambo ya kujifanya nimekunywa Mkuyati nikayaacha kabisa…

Nashukuru huyu mwanangu King'asti alikuwa akisoma boarding Secondary School, la sivyo kwa jinsi alivyo mnoko pangechimbika aisee……..!

Post a Comment

Previous Post Next Post