MZEE YUSSUF ABADILISHA KAMPUNI YA KUMTENGENEZEA VIDEO


KUNDI la Jahazi Modern Taarab chini ya Mzee Yussuf limeachana na kampuni iliyokuwa inatengeneza video za kundi hilo, Dolphin Production na kuhamia Shark’s (T) Limited.
Dolphin ndio kampuni iliyohusika kutengeneza karibu video za albam zote za Jahazi.
Mzee Yussuf ameiambia Hisia kuwa lengo la kuhama kampuni ni kujaribu kutafuta changamoto mpya lakini hana tatizo lolote na Dolphin.
“Tumefanya kazi vizuri na Dolphin na hajawahi kutuangusha, ila tunajaribu kuwapa wapenzi wetu vitu tofauti” alisema Mzee Yussuf.
Kwa hivi sasa Shark’s wanaendelea na uchukuaji wa video za albam mpya ya “Wasi wasi wako”.

Post a Comment

Previous Post Next Post