KOCHA Roberto Mancini ameponda sheria ya
kuzuia matumizi makubwa ya fedha, ambayo anaamini inaletwa ili
kupunguza nguvu ya klabu kama Manchester City.
Huku sheria mpya ya Ligi Kuu juu ya
matumizi ya fedha ikitarajiwa kutambulishwa ifanye kazi sambamba na
UEFA, itazipa wakati mgumu klabu kama City kufanikiwa bila kuwekeza.
'Sikubaliani,' alisema Mancini. 'Ikiwa
mimi ni tajiri, nataka kutumia fedha zangu zote timu yangu. Sikubaliani
na hii kwa ujumla, lakini hayo ni maoni yangu binafsi.
Angalia video huko chini
Roberto Mancini (kulia) akizungumza na Sergio Aguero
VIDEO Mancini asema mechi ya Real Madrid itawadhoofisha wapinzani wao, Man United


Post a Comment