
Post hii ni maalum kukuletea
taarifa kwamba february 10 2013 Maisha Club, yani jumapili hii ndio Ommy
Dimpoz staa ambae single yake ndio namba 1 kwenye Clouds Fm top 20,
anaikabidhi video yake mpya kwa Watanzania.
Ni video ambayo ameifanya Kenya na ni video yake ya kwanza kuifanya nje ya mikono ya Visua Lab ya Adam Juma.
Ni single ya Me and You aliyompa shavu mtangazaji wa 102.5 Choice Fm Dar es salaam Vanessa Mdee.
Dimpoz anaendelea kuwa kwenye
headlines baada ya Dj Cleo wa South Africa kuthibitisha kwamba yuko tayari kufanya ile kolabo waliyowahi
kuizungumzia na Ommy.
Namkariri akisema “tulizungumza kuhusu hiyo kolabo lakini haikufanyika, ila niko tayari kuifanya wakati wowote”
Post a Comment