Mwendeshaji wa Kipindi cha
Ongea na Janeth kinachorusshwa na Clouds Tv na DStv Bi. Janeth Sostenesi
akisaini daftari la wageni katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi
katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni jijini Dar es
Salaam mara baada ya kuwasili kwa ajili kufurahi na watoto hao katika
sikukuu ya wapendanao pamoja na kukabidhi msaada.
Bi. Janeth Sostenesi akijaribu
moja ya bidhaa za mikono zinazotengenezwa na watoto wa kituo cha
Kiwohede. Kushoto Mratibu Mipango wa Kituo hicho Bi. Stella Mwambenja.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha
Kiwohede Bi. Justa Mwaituka akizungumza na Mtangazaji wa Kipindi cha
Ongea na Janeth pamoja Crew nzima inayotengeneza kipindi hicho kuhusiana
na maendeleo yaliyokwisha fikiwa mpaka sasa na mipango ya baadae ya
kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Mtangazaji wa kipindi cha
Ongea na Janet na crew yake wakiimbia na kufurahi pamoja na watoto wa
kituo cha Kiwohede siku ta Valentines Day.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho akitambulisha wageni kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa na
kituo hspo akitoa shukrani kwa Bi. Janeth Sostenese pamoja na Crew kwa
kuonyesha upendo wa dhati kitu ambacho ni adimu kwao kutokana na
mazingira waliyotoka.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ongea
na Janet akizungumza na watoto wa kituo cha Kiwohede ambapo amewataka
kudumisha upendo baina yao na kujiona kama watu wengine, pia amewaasa
kukazania elimu ambayo itawakomboa na kuweza kuwa kama yeye hapo baadae
na amewaahidi kuendelea kuwa nao pamoja.

Janeth Sostenesi na Crew nzima
ya Ongea na Janeth wakikabidhi msaada wa fedha taslim kwa mwakilishi wa
watoto hao ikiwa ni upendo wake katika siku hii ya wapendanao.

Baadhi ya Watoto wa kituo cha Kiwohede wakifurahia msaada huo kutoka kwa kipindi cha Ongea na Janeth.

Crew nzima ya Ongea na Janeth katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Kiwohede.

Janeth Sostenesi akishow love na Mkurugenzi Mkuu wa shirikila lisilo la kiserikali la Kiwohede Bi. Justa Mwaituka.





Post a Comment