JOHANNESBURG, AFRIKA KUJSINI
OSCAR
PISTORIUS amepata dhamana leo Ijumaa, na atakuwa nje hadi kesi yake ya
kudaiwa kumuua kwa kumiminia risasi mpenzi wake, Reeva Steenkamp
itakapoanza.
Mwanariadha
huyo mlemavu aliyeshiriki michezo ya Paralimpiki aliinamisha kichwa
chake na kuonesha ‘huzuni ya furaha’ wakati Hakimu Desmond Nair akitoa
uamuzi wake katika mahakama ya Pretoria.
Pistorius
aliwapungia watu wa familia yake ambao baadae walionekana wakisali
baada ya hakimu Nair kutangaza uamuzi wake baada ya dakika 90 za kusoma
maelezo mahakamani.
Pistorius,
26, ameshitakiwa kwa mauaji ya kukusudia dhidi ya mpenzi wake ambaye ni
mwanamitindo, akidaiwa kuyatekeleza Februari 14, mwaka huu – asubuhi ya
Siku ya Wapendanao.
Mwanariadha
huyo anasema alimfyatulia risasi kwa bahati mbaya mpenzi wake kwa
sababu alidhani ni mtu hatari aliyevamia nyumbani kwake.
Waendesha
mashitaka wanasema alidhamiria kumuua mpenzi wake na kumshitaki kwa
makosa ya mauaji ya kukusudia, wakisema ufyatuaji risasi ulikuka baada
ya majibizano baina ya wawili hao.
Nair
alimwachia kwa dhamana ya randi milioni 1 (dola 113,000 za Marekani),
zikiwamo dola 11,300 taslimu na kuthibitisha kwamba zilizobaki
zinapatikana.
Hakimu
huyo alisema kuwa ni lazima Pistorius ambaye atarudi kortini kwa mara
nyingine Juni 4, akabidhi pasipoti zake za kusafiria na pia bunduki
ambazo anamiliki.
“Pistorius pia hawezi kutoka nje ya Pretoria bila ruhusa ya ofisa anayehusika na masuala ya dhamana,” alisema hakimu Nair.
Marehemu Reeva Steenkamp
Hakimu huyo pia alimuamuru kutorudi katika nyumba yake, ambako mauaji ya Steenkamp yalifanyika.
Masharti mengine ni pamoja na mtuhumiwa huyo kutotumia kilevi au mihadarati.
Uamuzi
huo umekuja baada ya siku nne za mvutano kati ya waendesha mashitaka na
upande wa utetezi katika usikilizaji wa maombi hayo ya dhamana.
Post a Comment