| Bi Mwanahawa Ali |
HATIMAYE sasa ni rasmi kuwa kundi la taarab la Five Stars limeuzwa na sasa litakuwa chini ya kampuni ya Shark’s (T) Ltd.
Katibu
mpya wa kundi hilo, Said Mangush ameiambia Hisia za Mwananchi kuwa kundi hilo sasa
lipo chini ya Shark’s na tayari limewasainisha mikataba wanamuziki
wapya watakaogeuza kabisa sura ya kundi hilo.
Tangu ajali ya kundi hilo iliyouwa wasanii 13 mwaka juzi, Five Stars imeshindwa kusimama imara na ilikuwa ipo kama haipo.
Mangush
amesema miongoni mwa wanamuziki wengi waliosajiliwa na kundi lao ni
pamoja na waimbaji Bi Mwanahawa Ali, Sabaha Muchacho, Mosi Suleiman,
Salha Abdallah na Hammer Q.
Post a Comment