ARSENE WENGER amesisitiza kuwa hajafikiria hata kwa sekunde moja suala la yeye kujiuzulu kuikochi Arsenal.
Kibarua
cha Wenger kiliingia doa katikati ya wiki kufuatia kipigo cha 3-1
kutoka kwa Beyern Munich katika mchezo wa ligi ya mabingwa ikiwa ni
pamoja na kutolewa na Blackburn kwenye kombe la FA.
Wenge,
63 anayejiandaa kumaliza msimu wa nane mfululizo bila taji lolote
alijibu kwa hasira pale alipoulizwa mapema wiki hii kuhusu hatma yake.
Lakini
jana katika mkutano wake na waandishi wa habari, akiwa amejaa utulivu
Mfaransa huyo alisema ana utashi wa kuendelea kuitumikia Arsenal kuliko
kipindi chochote kile.
Post a Comment