SITEGEMEI MWANAUME KAZI NDIO KILA KITU KWANGU - ODAMA

Jenifa kyaka (Odama)

Mwanadada nyota kutoka bongo movie Jenifa Kyaka Odama amefunguka na kusema katika maisha yake hategemei wanaume na ndio siri ya mafanikio aliyo nayo kwa sasa

Mwanadada huyo amesema anashukuru Mungu kwa kila hatua anayopiga na kwa sasa amejipanga kuhakikisha anafanya vizuri sana katika tasnia hii ya filamu hapa nchini.


Odama amekanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa mambo yote anayofananya ni msaada kutoka kwa pedeshee flan hapa mjini na badala amesema kila kinachoonekana ni juhudi zake binafsi na hakuna mkono wa mwanaume unajua watu wakimuona mwanamke kafanikiwa wanadhani ni nguvu ya mwanaume kiukweli hili huwa linaniumiza sana na ndio sababu tosha inayonifanya nisonge kila kukicha.


Hapa akikagua camera

Mwana dada Odama ameendelea kusema kuwa anajua anachokifanya hivyo haoni sababu ya kuongozwa na mtu mwingine,
Amesema anafanya kazi kwa bidii sana na ndio maana alisafiri kwenda china kwa ajili ya mahitaji ya kampuni yake ya J-FILIM 4 LIFE Ambayo imeshatengeza filamu kibao zinazofanya vyema sana dukani kwa sasa


Odama ametoa wito kwa wasanii wachanga na hata mastaa kuwa hakuna kitu kizuri kama kujituma kwani unapofanya kazi kwa bidii basi jua pesa zitamiminika tu ila ukikaa na kupiga domo basi utaishia domo kwani pesa zinatafutwa na hazitutafuti sisi..Nachoshauri kina dada wenzangu tufanye kazi tukikaa na kusema bila vitendo tutabaki kilalamika kila siku maana hakuna kitu kibaya na adui wa pesa kama uvivu.Odama alizidi kutiririka na kusema kama kuna wanawake haswa mastaa wenye tabia za kuwa tegemezi waache kwani siku wakigombana wajue ndio mwisho wa kupata pesa ila ukiwa na chako huwezi kuteseka.


Akiendelea kununua

Kwa sasa mwanadada huyu amesema anajipanga na atafanya fila kubwa na ya historia ambayo itakayotumia gharama kubwa sana kwa wengi wawatakaoshiriki watatoka nje ya nchi bila kufafanua nchi gani na wanaotoka nje wanakuja kama wasanii au crew.

Kwasasa Odama anamiliki biashara zake na ana mipango kibao ambayo itakamilika muda si mrefu kama mungu akitujalia na kila mtu atajua Odama anataka kufanya
Wakizungumza na sisi kwa nyakati tofauti mashabiki wa filamu wamesema wanamkubali sana mwandada huyu kwani anakwepa sana kuandikwa kwa habari za uwongo pili wanamkubali kwani ni mwanadada mpiganaji mwenye ndoto kubwa sana za maisha bora.


Hapa akikagua stick ya boom

Odama amefunguka kuwa ana amini filamu aliyoifanya na kuwashirikisha Riyama Ally, Cath na wasanii wengine wengi itafanya vizuri sana sokoni kwani ni filamu nzuri na ina mafunzo na ana amini itapendwa sana kwani watu waliocheza wamefanya vizuri sana

Post a Comment

Previous Post Next Post