SONG NA ETO'O KUIKOSA STARS KESHO


Football | Tanzania

Alex Song @ Getty Images

Song kuikosa Tanzania kesho


KIUNGO wa Barcelona Alex Song na mshambuliaji Samuel Eto'o wa Anzhi Mkhachkala ya Urusi, hawatakuwepo kwenye mechi ya kesho baina ya timu yao ta taifa, Cameroon dhidi ya wenyeji Tanzania.
Taarifa nchini Hispania zimesema kiungo huyo wa zamani wa Arsenal anasumbuliwa na maumivu ya goti na hatakuja kabisa.

Song alitarajiwa kutua Dar es Salaam leo asubuhi kuungana na wenzake tayari kwa mchezo huo.

Cameroon imekosa tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutolewa na Cape Verde, ambapo walikomea Robo Fainali.

Kikosi cha Cameroon sasa kinachotarajiwa kushiriki mchezo wa kesho ni Charles Itandje, Mayebi Joslain, Allan Nyom, Benedict Angbwa, Benoît Assou Ekotto, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Armel Kana Biyick, Bouba Aminou, Joel Matip, Nguemo Landry, Pierre Wome Nlend, Hervé Tchami, Fabrice Olinga Essono, Achille Emana, Eloundou Charles, Jean Makoun II, Vincent Aboubakar na Jean Paul Yontcha.
© supersport.com

Post a Comment

Previous Post Next Post