"TAFF NA BONGO MOVIE HATUNA UGOMVI"..MWAKIFAMBA




RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba ashangazwa na baadhi ya wadau kudai shirikisho hilo, limekuwa na malumbano ya chini na Kampuni ya Wasanii Tanzania BongoMovie.

Kampuni ya Bongomovie, inaundwa na wasanii 11 maarufu wanaotengeneza filamu nchini.

Hivi karibuni ilidaiwa kwamba kuna baadhi ya wasanii nchini, hawana imani na TAFF hasa katika michango inayotolewa katika misiba na matamasha, yanayoandaliwa na wasanii hao ambao wapo chini ya shirikisho hilo.

Kutokana na hali hiyo Mwakifwamba, amevunja ukimya na kulimwagia data  kwamba TAFF na kampuni hiyo BongoMovie, hakuna malumbano yoyote na kila kitu kipo safi kati yao.

"Tangu lini Taasisi ikalumbana na kampuni, hakuna kitu cha namna hiyo labda kampuni inaweza kulumbana na kampuni nyingine, taasisi inaweza na chombo kingine kinacho lingana hadhi hiyo," alisema Mwakifamba.

Post a Comment

Previous Post Next Post