Mshambulia wa Polisi Morogoro Nohoda
Bakari akiwania dhidi ya mlinzi wa African Lyon ya Jijini Dar es Salaam,
Hood Mayanja kulia wakati wa mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania
bara uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo
huo African Lyon ilikubali kipigo cha bao 1-0 na kuendelea kuburuza mkia
katika mzunguko huu wa pili wa ligi hiyo.
Mlinda Mlango wa African Lyon Abdul
Seif kulia akidaka mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Polisi
Morogoro Keneth Masumbuko wakati wa mchezo wao.
Mlinzi wa African Lyon Ibrahim Issac kulia akipiga mahesabu ya kumzuia mshambuliaji wa Polisi Morogoro Tizo Chomba kushoto.
Mshambuliaji wa Polisi Morogoro Keneth
Masumbuko ambaye alikuwa akisumbua ngome ya African Lyon kushoto
akimtoka mlinzi wa timu hiyo Ibrahim Issac ili kupeleka mashambulizi
katika lango wa wapinzania wao.
Askari wa kuliza ghasia wakiwa
wanawapa ulinzi waamuzi wa mchezo huo chini ya mwamuzi wa kati Andrew
Shamba wa Pwani mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao wenyewe
waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Benchi la ufundi la African Lyon
likiongozwa na kocha mkuu Charles Otien wa kwanza kushoto wakati
wakishuhudia jahazi likizama dhidi ya maafande wa Polisi Morogoro kwa
kukubali kutwandikwa bao 1-0.
Benchi la ufundi la Polisi Morogoro chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Mohamed Richard
wa pili kutoka kushoto ambapo walifanikiwa kuliongoza vema jahazi lao
dhidi ya African Lyon na kuibua kidedea kwa bao 1-0.
KIKOSI CHA AFRICAN LYON.
KIKOSI CHAPOLISI MOROGORO.
Wachezaji wa polisi Morogoro wakiwasalimia wachezaji wa African Lyon muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wao.
Hapa waamuzi wakiwaongoza wachezaji kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kuingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo huo.
Post a Comment