Na Bosire Boniface amechangia katika ripoti hii kutoka Wajir
![]() |
Kutoka juu kushoto, kuelekea mbele:
Wycliffe Musalia Mudavadi, Martha Wangari Karua, Peter Kenneth, Mohammed
Abduba Dida, Paul Kibugi Muite, Raila Amollo Odinga, Uhuru Muigai
Kenyatta, na James ole Kiyiapi.
|
Kwa kuwa uchaguzi wa Kenya umepangwa kufanyika tarehe 4 Machi, Tume Huru
ya Uchaguzi na Mipaka imetangaza wagombea wanane watakaoshindania
nafasi hizo za juu za nchi. Ufuatao ni wasifu wa kila mgombea wa urais,
wamepangwa kialfabeti.
Mohammed Abduba Dida
Mohamud Abduba Dida alizaliwa mwaka 1975 katika wilaya ya Wajir. Dida,
aliyekuwa mwalimu, anagombea urais kupitia Muungano kwa ajili ya
Mabadiliko Halisi (Alliance for Real Change). Mgombea mweza wake ni
Joshua Odongo Onono, pia alikuwa mwalimu.
Dida, mpya katika siasa, ameapa kuwa Rais ambaye ataawangalia maskini.
Alisema elimu inapaswa kuwa bure kwa Wakenya wote, na siyo kwa kutegemea
mfumo wa ruzuku. Dida ameelezea kwa kujiamini kwa uwezo wake wa kufanya
vizuri katika uchaguzi, kama alivyosema chama chake kinaungwa mkono
sana na vijana.
![]() |
| Mohammed Abduba Dida. [Jalada] |
Ana digrii ya elimu kutoka chuo kikuu cha Kenyatta na kwa sasa anafanya
digrii ya uzamili katika masomo ya dini kutoka chuo kikuu cha Nairobi.
Dida amefundisha katika shule kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufundisha
fasihi ya Kiingereza na dini katika shule ya sekondari ya Daadab katika
kambi mchanganyiko ya wakimbizi na baadaye katika shule ya Lenana.
![]() |
| Martha Wangari Karua. [Tony Karumba/AFP] |
Alijiuzulu kufundisha mwaka 2009 na kuanza kazi ya uwakala wa kazi ya
muda, lakini alisema mradi haukufanikiwa kwa sababu ya rushwa ya
serikali.
Martha Wangari Karua
Martha Karua, mgombea pekee mwanamke, katika kinyang'anyiro cha urais,
alizaliwa Septemba 1957 huko Kirinyaga, Jimbo la Kati. Karua, mbunge wa
Gichugu, anagombea kupitia National Rainbow Coalition pamoja na
aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Bunge la Afrika Mashariki Augustine
Lotodo.
![]() |
| Peter Kenneth. [Jalada] |
Wakati wa mjadala wa urais, alisema atashughulikia kima cha juu cha vifo
vinavyotokana na uzazi kwa kutoa upatikanaji wa huduma za afya mahali
kote.
![]() |
| Uhuru Muigai Kenyatta. [Simon Maina/AFP] |
Karua ana digrii ya sheria kutoka chuo kikuu cha Nairobi na digrii ya
uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani, Nairobi.
Kuanzia mwaka 1981 hadi 1987, Karua alifanya kazi mahakamani, alipanda
kutoka hakimu wa wilaya hadi hakimu mkuu mkazi. Baada ya hapo amekuwa na
shirika la uwakili binafsi hadi 2002.
Mwaka 1992, Karua alichaguliwa kuwa mbunge wa Gichugu, kiti ambacho anakishikilia hadi sasa.
![]() |
| James ole Kiyiapi. [Tony Karumba/AFP] |
Mwaka 2009, Karua alijiuzulu katika nafasi yake ya uwaziri katika
serikali ya umoja akitaja kukatishwa tamaa katika kutekeleza kazi zake.
Peter Kenneth
![]() |
| Wycliffe Musalia Mudavadi. [Jalada] |
Kama mgombea, Kenneth amejielekeza katika kuboresha tatizo la ukosefu wa
ajira na uhakika wa chakula. Pia alidhamiria kuipa polisi vifaa na
kuwalipa vizuri maofisa ili kuwahamasisha kufanya kazi nzuri, na
anaamini kwamba maendeleo na elimu katika maeneo yanayokumbwa na uhalifu
yatazuia vitendo haramu. Anapanga kulipia programu zake kwa kupunguza
matumizi makubwa ya serikali.
Kenneth ana shahada ya kwanza na ya uzamili katika sheria kutoka Chuo
Kikuu cha Nairobi, pamoja na kozi ya shahada ya juu kutoka Taasisi ya
Kimataifa ya Programu ya Utendaji kwa ajili ya Maendeleo ya Usimamizi
huko Lausanne, Uswizi.

Paul Kibugi Muite. [Jalada]
Kama mkurugenzi wa benki, Kenneth alianza kufanya kazi na Kampuni ya
Fedha ya Nationwide mwaka 1985, kisha akafanya kazi na Prudential
Finance na Benki tangu 1986 hadi 1997, ambako alikuwa meneja. Kuanzia
1997 hadi 2002, alifanya kazi katika Kampuni ya Kukata Bima ya Kenya,
wakati huo huo akishika vyeo katika Shirika la Kukata Bima la Afrika na
Benki ya Maendeleo ya Viwanda. Tangu 1998 hadi 2009, alifanya kazi kama
mwenyekiti wa Kampuni ya Kukata Bima ya Zep.
Katika maisha yake ya kisiasa, Kenneth alichaguliwa kwa mara ya kwanza
kama mbunge wa kiti cha Gatanga mwaka 2002, kiti anachokishikilia hadi
sasa.
Tangu 2003 hadi 2005, alifanya kazi kama msaidizi wa waziri katika
Wizara ya Maendeleo ya Ushirika na Masoko, kisha kama msaidizi wa waziri
katika Wizara ya Fedha hadi 2007. Tangu 2008, amekuwa msaidizi wa
waziri katika Wizara ya Mipango, Maendeleo ya Taifa na Dira ya 2030.

Raila Amollo Odinga. [Will Boase/AFP]
Uhuru Muigai Kenyatta
Uhuru Muigai Kenyatta alizaliwa Oktoba 1961. Baba yake ni rais wa kwanza
wa Kenya Jomo Kenyatta, ambaye aliongoza tangu 1964 hadi 1978. Ni
mgombea wa urais wa chama cha Jubilee Alliance, chama cha muungano
kilichoundwa chini ya The National Alliance cha Kenyata na chama cha
United Republican cha William Ruto.
Katika ilani ya muungano wake, Kenyatta ana msimamo wa Kenya iliyoungana
"chini ya ndoto moja ya kujenga Kenya bora". Alisema atajikita katika
suala la umiliki wa ardhi, na anadhamiria kuibadili Kenya kuwa kitovu
cha uchumi, akijenga uchumi wa usafirishaji bidhaa nchi za nje.
Kenyatta ana shahada ya kwanza katika siasa na uchumi kutoka Chuo cha Amherst huko Marekani.
Baada ya kipindi kifupi cha kufanya biashara, Kenyatta aligombea kiti
cha ubunge cha Gatundu Kusini mwaka 1997, lakini alishindwa. Miaka
miwili baadaye, Rais Daniel arap Moi alimteua kuwa mwenyekiti wa Bodi ya
Utalii ya Kenya, na mwaka 2001, alimteua bungeni.
Kenyatta aligombea urais bila ya mafanikio mwaka 2002, lakini alishinda
kiti cha ubunge akiwakilisha Gatundu kusini mwaka huohuo.
Aligombea urais tena mwaka 2007, lakini alijitoa na kumuunga mkono Rais
Mwai Kibaki kwa uchaguzi wake tena. Kibaki alimteua Kenyatta waziri wa
serikali za mitaa mwezi Januari 2008 kabla ya kuwa naibu waziri mkuu na
waziri wa biashara mwezi Aprili 2008 kama sehemu ya serikali ya umoja
iliyopanga kumaliza vurugu baada ya uchaguzi 2007.
Alihamishiwa katika Wizara ya Fedha kuanzia mwaka 2009 hadi 2012, wakati
akiendelea kuwa naibu waziri mkuu. Aliacha kazi ya uwaziri wa fedha
mwezi Januari 2012 baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
(ICC) kumtuhumu kwa kufanya uhalifu kinyume cha ubinadamu kwa wajibu
wake katika vurugu za uchaguzi wa 2007-2008.
Wote Kenyatta na Ruto walikabiliwa na upinzani wakati wa kampeni za
uchaguzi kuhusiana na kesi zao zilizosimamishwa na ICC, na Kenyatta
alijibu maswali kuhusiana na suala hili wakati wa mdahalo wa urais.
James ole Kiyiapi
James ole Kiyiapi alizaliwa mwezi Mei 1961 huko Osupuko, Jimbo la Bonde
la Ufa. Katibu Mkuu wa zamani katika wizara mbalimbali, aliacha kazi
mwaka 2012 ili kugombania pamoja na mwanamke mfanya biashara Winnie
Kaburu chini ya Urejeshaji na Kukijenga chama cha Kenya Party.
Kiyiapi anasimamia ilani ya uchaguzi inayokana siasa za kikabila.
Alisema kipaumbele chake cha awali kitakuwa kuzingatia ukosefu wa ajira
kwa vijana, ambalo aliita janga la taifa. Serikali yake, alisema,
itashinikiza kazi ya kumaliza migogoro ya ardhi kwa uangalifu wa hali ya
juu na uwazi, na itaboresha uzalishaji wa kilimo nchini.
Kiyiapi ana shahada ya uzamili kutoka katika Chuo Kikuu cha Moi na
shahada ya uzamivu kutoka katika Chuo Kikuu cha Toronto nchini Kanada,
zote ni kuhusu misitu.
Kuanzia mwaka 1988 hadi 1994, alikuwa mtafiti mwandamizi katika kitivo
cha Utafiti wa Mazingira katika Chuo Kikuu cha York nchini Kanada.
Alifanya kazi kama mhadhiri na Profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha
Moi kuanzia mwaka 1994 hadi 2006.
Wakati huo, pia alifanya kazi kama mkurugenzi wa programu nchini katika Mfuko wa Wanyamapori Afrika.
Kiyiapi aliteuliwa kuwa katibu mkuu katika Wizara ya Mazingira na
Maliasili mwaka 2006, Wizara ya Huduma za Tiba mwaka 2008, na Wizara ya
Elimu mwaka 2010.
Wycliffe Musalia Mudavadi
Naibu Wairi Mkuu Wycliffe Musalia Mudavadi alizaliwa mwezi Septemba 1960
huko Sabatia, Jimbo la Magharibi. Anagombea kupitia chama cha United
Democratic Forum katika Amani Alliance, pamoja na Jeremiah Kioni, mbunge
kutoka Jimbo la uchaguzi la Ndaragwa.
Mudavadi ameahidi kukuza uchumi wa uhakika nchini Kenya kwa kuzingatia
utawala bora na kupunguza umaskini. Alisema atakabiliana na rushwa
nchini kwa kupanga upya mfumo wa mahakama, na kuajiri maofisa polisi
wengine zaidi ili kuboresha usalama.
Mudavadi ana shahada ya uchumi wa ardhi kutoka katika Chuo Kikuu cha
Nairobi. Baada ya kuhitimu, alifanya kazi katika Shirika la Nyumba la
Taifa kabla ya kufanya kazi katika kampuni ya Tysons Limited inayohusika
na ujenzi na upangishaji wa nyumba.
Mudavadi alikuwa mbunge mwaka 1989, wakati alipochaguliwa bila kupingwa
kuchukua kiti cha ubunge wa Sabatia kilichoachwa wazi baada ya kifo cha
baba yake, Moses Mudavadi.
Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1992, Mudavadi aliteuliwa kuwa waziri wa
fedha kwa miaka mitano. Mwaka 1998, aliteuliwa kuwa waziri wa kilimo,
kisha waziri wa habari, uchukuzi na mawasiliano mwaka 1999, na waziri wa
uchukuzi na mawasilino mwaka 2001. Kwa kipindi chote hiki alishikilia
kiti cha ubunge wa Sabatia.
Mwaka 2002, Mudavadi alipoteza kiti chake cha ubunge, lakini aliteuliwa
na Rais Daniel arap Moi kuwa makamu wa rais na alishikilia nafasi hiyo
kwa miezi miwili. Kisha aligombea bila mafanikio nafasi ya makamu wa
rais na mgombea mwenza Uhuru Kenyatta mwaka 2002.
Baada ya hapo, Mudavadi alisaidia kuanzisha chama cha Orange Democratic
Movement na aligombea kwa nafasi ya rais wa chama mwaka 2007, lakini
Raila Odinga alimshinda.
Tangu hapo, alikuwa akifanya kazi kama mjumbe wa Bodi ya Magavana wa
Benki ya Dunia na mjumbe wa Kamati ya Bunge iliyochaguliwa kwa ajili ya
Mabadiliko ya Katiba.
Mwaka 2012, Mudavadi aliondoka katika chama cha Orange Democratic
Movement na kujiunga na chama cha United Democratic Front. Kwa muda
mfupi alijiunga na chama cha Jubilee Alliance cha Uhuru Kenyatta, lakini
aliamua kujitenga mwezi Desemba baada ya kutokubaliana kuhusu nani
atakayeongoza.
Paul Kibugi Muite
Paul Kibugi Muite alizaliwa mwezi wa Aprili 1945. Ni mbunge wa zamani
kutoka Kabete ambaye ni mwanachama muanzilishi na kiongozi wa Chama cha
Safina. Anagombea pamoja na Shem Ochuodho, waziri wa zamani wa nishati
na mbunge kutoka Rangwe.
Muite alisema, yeye kama rais atashughulikia ukosefu wa ajira na
kuboresha hali za kazi, sehemu moja kwa kupandisha mishahara na
kuimarisha sheria za kazi ambazo zinaweka kikomo cha saa siku ya kazi
kuwa masaa manane. Pia aliapa kuzuia ufisadi wa serikali, jambo
alilosema kuwa "limewapeleka mamilioni ya Wakenya katika umasikini wa
milele na mateso".
Anasema anaamini kwa umoja wa Wakenya wote, bila ya kujali makabila yao,
na atafanyia kazi uboreshaji jamii na uchumi kwa watu wote. Muite
anasema Kenya pia inaumizwa na sifa hasi kimataifa kwa ufisadi na rekodi
mbaya ya haki za binadamu, jambo ambalo ameahidi kulishughulikia
kupitia elimu na masoko.
Muite, mwanasheria wa haki za binadamu, alikuwa mtu maarufu wakati wa
siku za mwisho za mfumo wa chama kimoja miaka ya 1990, ambayo
ilianzishwa na Kenya African National Union (Chama cha Kitaifa cha
Waafrika wa Kenya) mwaka 1982.
Alitumikia vipindi vitatu vya miaka mitano mitano kama mbunge wa Kabete, mwaka 1992, 1997 na 2002.
Raila Amollo Odinga
Waziri Mkuu Raila Amollo Odinga alizaliwa tarehe 7 Januari mwaka 1945
huko Maseno Jimbo la Nyanza, mtoto wa Makamu wa Rais Jaramogi Oginga
Odinga. Anagombea katika chama cha Orange Democratic Movement (Harakati
Kidemokrasia za Chungwa) pamoja na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka kama
mgombea wake mwenza.
Odinga amejikita katika vijana kwenye kampeni zake, akiwaahidi kupata
ajira na elimu. Alisema kuwa atatoa pesa taslimu kwa masikini na wazee,
na kuanzisha mpango kwa vijana wanaosubiri kuingia chuo kikuu au
wanaotafuta kazi kwa kufundisha kwenye shule za msingi.
Kiuchumi, alisema ataanzisha progamu za kusafirisha bidhaa
zinazotengenezwa vijijini nchini Kenya, na kusaidia ukuaji wa sekta ya
chuma cha pua. Alisema kuwa ataboresha miundombinu na kupanua uwekezaji
katika usalama wa chakula kupitia kilimo kilichoboreshwa, ruzuku kwa
wakulima na utafiti.
Odinga anayo shahada ya uzamili ya uhandisi mitambo kutoka Chuo cha
Magdeburg Cha Tekonolojia ya Juu. Pia ametunukiwa digirii za heshima za
uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufundi
cha Florida huko Tallahassee, Marekani.
In 1970, alianza kufanyakazi kama mhadhiri kwenye idara uhandisi mtambo
katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1974, aliondoka wakati alipoteuliwa
kama meneja wa viwango katika kikundi kwenye Ofisi mpya ya Viwango ya
Kenya, ambako alikuwa naibu Mkurugenzi mwaka 1978.
Mwaka 1982, Oginga Odinga alihusishwa kama mtoa fedha wa jaribio la
mapinduzi dhidi ya serikali ya Raisi Daniel arap Moi, ambaye alikuwa
amezuwia jaribio la Oginga Odinga la kusajili chama cha upinzani. Raila
Odinga alishitakiwa kwa uhaini na kuwekwa kuzuizini kwa muda wa miaka
sita bila kesi.
Odinga aliachiwa huru mwaka1988, lakini na kutiwa mbaroni tena mwaka
mmoja baadaye kwa kuhusika na Harakati za Mapinduzi Kenya, kikundi
kilichokuwa kkinashinikiza kuwepo kwa demokrasia ya vyama vingi nchini
Kenya.
Odinga alikamatwa tena mwaka 1990 na alipoachiwa huru mwaka 1991 aliomba
hifadhi huko Norway, kwa madai kwamba serikali ilikuwa inapanga kumuua.
Baadya ya mwisho wa mfumo wa chama kimoja, Odinga alirejea mwaka 1992 na
kujiunga na Jukwaa la Demokrasia (FORD), chama cha siasa kilichokuwa
kinaongozwa na baba yake, na kushinda kiti cha ubunge katika eneo la
ubunge la Langata.
Mwaka wa 1997, Odinga alishindwa alipogombania urais.
Odinga alifanyakazi kama waziri wa nishati kutoka mwaka 2001 hadi 2002
na kama waziri wa barabara, kazi za umma na nyumba kutoka mwaka 2003
hadi mwaka 2005.
Mwaka 2005, Odinga aliondoka FORD na kuasisi chama cha Democratic
Movement, ambako aligombea bila mafanikio mwaka 2007. Baada vurugu
iliyofuatia, Odinga akawa waziri mkuu katika serikali ya kugawana
madaraka.

![Mohammed Abduba Dida. [Jalada]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/02/15/kenya-mohammed-dida-340_227.jpg)
![Martha Wangari Karua. [Tony Karumba/AFP]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/02/15/kenya-mary-karua-340_227.jpg)
![Peter Kenneth. [Jalada]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/02/15/kenya-peter-kenneth-340_227.jpg)
![Uhuru Muigai Kenyatta. [Simon Maina/AFP]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/02/15/kenya-uhuru-kenyatta-340_227.jpg)
![James ole Kiyiapi. [Tony Karumba/AFP]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/02/15/kenya-james-kiyiapi-340_227.jpg)
![Wycliffe Musalia Mudavadi. [Jalada]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/02/15/kenya-musalia-mudavadi-340_227.jpg)
Post a Comment