
| Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) |
Najua
kama umekua karibu na media katika siku za karibuni, stori kuhusu
uongozi wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza mpango wa
kutaka bunge lisiwe linaonekana live kwenye TV utakua umeisikia.
Ni
maoni mengi ya Watanzania yametolewa huku asilimia kubwa ikionekana
kupinga huo mpango ambao lengo lake ni kukwepa kuonekana kwa wabunge
wanaovunja kanuni kwa kuropoka na kufanya vurugu.
Kwenye
hii post ni maoni maalum ya mbunge wa Kawe Halima Mdee ambae namkariri
akianza kwa kusema “mmhh… kwanza ni hoja ya kipuuzi sana na muhimu
ikaeleweka kwamba bunge ni moja kati ya mihimili mitatu ya dola,
kinachoonekana kutaka kufanyika ni muhimili mwingine wa dola kutokutaka
umma ujue ukweli kwa kutumia watumishi wa bunge kwa mantiki ya katibu wa
bunge kwa sababu yeye ndio ametoa hilo tamko ili kuzuia Watanzania
wasipate taarifa ambazo tokea bunge limeanza kurushwa live wamekua
wakizipata tofauti na ambavyo walikua wanapewa hizo taarifa katika
mazingira ambayo sio ya wazi”
Kwenye
sentensi nyingine Mh Mdee amesema “nasema hivyo kwa sababu kupitia
bunge Watanzania wamejua mikataba mibovu ya madini, wamejua EPA, wamejua
Richmond, Buzwagi, wamejua jinsi gani fedha zinavyotengwa kwa ajili ya
bajeti zimekua zikitumika vibaya sana kupitia CAG report ambazo zimekua
zinajadiliwa live, Serikali imeona inaumbuka na ikaamua sasa kupitia
katibu wa bunge na kina Lukuvi, tunataja majina ya watu sababu tuna
uhakika na tunachokisema na juzi imeumbuka, sasa wanatafuta statergy ya
kuficha”
“Kama
mlikua mnafatilia bunge la juzi mmeona kwamba wameweka sheria kusema
kwamba mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG taarifa yake akiisoma
haitajadiliwa hadi mwaka tena mwingine upite waende tena kuedit na
kuleta majibu ya uongo, kwa hiyo kuna mrundikano wa vitu vingi ambavyo
Serikali inaona mambo yakiendelea hivi inawezekana 2015 wakifika watakua
wamechoka, sasa wanazuiaje? kwa kuleta vitu vya ajabu ajabu… kwa hiyo
waache wananchi wajue nini kinachoendelea, kuna kanuni za bunge kama
Mbunge anakiuka kanuni” – Halima Mdee
Post a Comment