![]() |
| Viongozi wa SADC katika moja ya vikao jijini Dar Es Salam |
Rais wa msumbuji Armando Guebuza ameitisha kikao cha dharula
cha viongozi wa jumuiya kicuhumi ya nchi za kusini mwa bara la Afrika
SADC jiji Maputo Ijumaa hii, ili kujadili kuhusu hali ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo. Viongozi wa Ikulu ya rais nchini Msumbuji
wamesema kwamba mkutano huo utajadili kuhusu maendeleo ya kisiasa nchini
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo bila hata hivo kutokwa muelezi
zaidi.
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete kiongozi wa kamati ya
Usalama na Ulinzi ya SADC na rais wa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
DRC Joseph Kabila wametangaza kushiriki kikao hicho.
Wajumbe mkutanoni watajaribu kujadili kuhusu tofauti zolizopo katika
SADC kuhusu kutumwa kwa vikosi vya kulinda amani mashariki mwa DRCongo,
suala ambalo linaonekana kukwamisha kusaini makubaliano ya amani
yalioitishwa na Umoja wa Mataifa.
Duru za kidiplomasia zinaarifu kuwa nchi tatu ambazo zipo tayari
kutuma vikosi vyao huko mashariki mwa DRCongo, Afrika Kusini, Tanzania
na Msumbuji zinataka kuwa huru katika uongozi na sio kuwa chiniya
uongozi wa Umoja wa Mataifa.
Kikosi cha huduma za haraka chenye kuundwa na wanajeshi 2.500 ambacho
Umoja wa Mataifa unataka kuunda kinatakiwa kuwa na uwezo wa kuingilia
haraka iwezekanavyo, badala ya ilivyo kwa sasa na vikosi 17.000 vya
operesheni ya Umoja wa Mataifa MONUSCO vikiwa na majeshi ya FARDC,
lakini pia vikiwa pekeavyo vikijitegemea kwa uwezo maalum.
Jeshi la Congo FARDC linapambana tangu mwezi April 2012 na kundi la
waasi wa M23, waasi ambao Umoja wa Mataifa unasema waungwa mkono na
Rwanda na Uganda.
Mzungumzo ya amani yanaendelea huko Kampala Uganda baina ya wajumbe wa serikali na waasi wa m23

Post a Comment