Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la
HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na
idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa
serikali inafikiria warudie mtihani mwaka huu.
Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.
Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.
Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema, matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu
Post a Comment