Waumini 22 wa Kihundu nchini India wamekufa baada ya kutokea mkanyagano

Watu wasiopungua 22 wamekufa katika mkanyagano kwenye mji wa Allahabad, baada ya umati mkubwa wa waumini wa madhehebu ya Hindu waliokuwa wakitoka kujitakasa kwenye makutano ya mito ya Ganges na Yamuna, kulivunja daraja dogo kwenye kituo cha Reli.
Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh amesema ameshtushwa na tukio hilo na kuahidi kutoa msaada wa kifedha kwa familia za wafiwa.
Mamilioni ya wahindu walishiriki katika sherehe zinazojulikana kama Maha Kumbh Mela, ambazo ni takatifu zaidi kwa mujibu wa imani yao.
Wahindu huamini kuwa kuoga maji ya mito hiyo huwaondolea dhambi na kuwakinga na mzunguko wa kuzaliwa katika maisha mapya.
Kila baada ya miaka 12, wahindu kutoka sehemu zote za India na kwingineko duniani hukusanyika mahali ambako mito ya Ganges na Yamuna hukutana na mto wa tatu wa kimiujiza.

Post a Comment

Previous Post Next Post