![]() |
| JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti. |
Watuhumiwa hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza Mwanza.
Baada ya
kunaswa kwa mtuhumiwa huyo, alisaidia kuwaelekeza polisi walipo wenzake,
ambao walikutwa katika hoteli moja jijini Mwanza wakiwa wamejipumzisha.
![]() |
| Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo. |
![]() |
Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa
vilivyokamatwa navyo ni kadi za bandia 194 za kuchukulia fedha katika
ATM za Benki ya NMB, ambapo kati yake kadi 95 zilikuwa na
namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina
na picha ya mtu anayedaiwa kuwa ni mtumiaji mwenye jina la Molely L. P.
Kadi nyingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti
namba 5068000322 zikitumia jina moja la Mnuo Z. E na picha moja.
|
Mbali
na kadi hizo pia waliweza kunasa kadi 36 za Benki za DTB, ambazo kati
yake kadi 18 zilikuwa na jina moja la Kelvin G. Gratias na namba 20497883,
kadi 12 zikitumia jina la John J. Paul zenye akaunti namba 2049783 huku
kadi sita zikitumia jina moja la Joseph Donald akaunti namba 2049783.
Kadi
nyingine tatu zenye maandishi ya Download List na nyingine ikiwa ni kadi
ya Visa ya Benki ya KCB yenye namba 4183546040003827 zikitumia jina la
Elikana Zacharia. Kadi nyingine zilikuwa ni tupu zisizo na maandishi
wala nembo ya benki yoyote na nyingine zikiwa ni Soviet Royalty, kadi ya
raia ya Urusi ikiwa na namba 000724.
![]() |
| Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell. |
Walikamatwa
pia wakiwa na vifaa mbalimbali vya kielektroniki ikiwamo kamera za siri
tatu za kienyeji ambazo zimetengenezwa kwa kufungwa betri za simu ya
mkononi na pia walikamatwa na kifaa cha kutengenezea kadi bandia
(Magnetic Card reader), mikebe mitatu ya rangi za kupulizia kamera za
usalama katika ATM ili wasionekane wakati wa wizi wao, ‘printer’ pamoja
na kifaa cha kuchomea vifaa vya umeme.
![]() |
Wizi ulivyofanyika
Wahalifu
hufika katika mashine za kutolea fedha ambapo hatua ya kwanza ni kuzima
kamera za usalama za eneo husika kwa kuzipulizia rangi maalumu ili
kuzitia ukungu hivyo kuharibu mwonekano wake na kuruhusu wao kuingia
eneo hilo bila ya kuonekana na kufanya wizi wao.
|
Mara
baada ya kuziharibu kamera za usalama, walikuwa wakianza kwa kuweka
kamera zao za siri ili kunasa namba za siri za kufungulia akaunti ambazo
huzisoma katika ‘kompyuta’ na kuzinakili katika daftari lao maalumu na
kisha kuchukua kadi zao bandia na kuchukua fedha.
Wizi huo
wa kuchukua fedha waliufanya nyakati za usiku saa sita hadi saa tisa
usiku wakati ule wa kutegea kamera zao ulifanyika muda ambao huwa na
wateja wengi hasa siku za mapumziko.





Post a Comment