
Waziri Mkuu wa Israeli, BenJamin Netanyahu
Na Flora Martin Mwano
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wa chama cha mrengo wa kushoto
pamoja na washirika wake katika serikali ya muungano toka mrengo wa
kulia wamefanikiwa kutupilia mbali changamoto zao baada ya kufikia
makubaliano ambayo yatashuhudia serikali mpya ijumaa hii.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kiongozi wa chama cha Yesh Atid, Yair
Lapid na Naftali Bennett wa Jewish Home wamelegeza msimamo wao katika
suala la Naibu Waziri Mkuu, suala ambalo lilikuwa kikwazo kikubwa katika
kufikia muafaka wa serikali ya muungano.
Baada ya makubaliano hayo serikali mpya inatarajiwa kuwasilishwa kwa
Rais Shimon Peres hapo kesho na baraza jipya la mawaziri linatarajiwa
kuapishwa mbele ya bunge jumatatu ijayo masaa 48 kabla ya Rais wa
Marekani Barack Obama kuzuru nchini Israel.
Wizara ya fedha na elimu inatarajiwa kuwa chini ya upande Yesh Atid
ambao walinyakua viti 19 vya bunge kati ya 120 katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Upande Jewish Home wanatarajia kuongoza wizara za viwanda na biashara
pamoja na ile ya makazi ambayo inahusika na ujenzi wa makazi ya Wayahudi
katika eneo lenye mgogoro kati ya Israel na Palestina.
Wizara ya mambo ya nje, ulinzi na mambo ya ndani zitakuwa chini ya
upande wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu ambaye muungano wake wa kisiasa
ulinyakua viti 31 katika uchaguzi wa wabunge.
Source: kiswahili.rfi.fr
Post a Comment