
BARAZA la
Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) limempa tuzo ya
heshima ya kuthamini mchango wake katika jamii aliyekuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),
Ananilea Nkya.
BAWACHA
ilitoa tuzo hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
yaliyofanyika juzi katika Ukumbi wa Don Bosco, Upanga jijini Dar es
Salaam.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa mgeni rasmi, Gema Akilimali kwa niaba ya Nkya ambaye yupo masomoni Uingereza.
Makamu
Mwenyekiti wa BAWACHA, Suzan Lyimo alisema walimzawadia tuzo hiyo
kutokana na kazi zake kwa jamii; haki za wanawake na watoto katika
matendo ya ubakwaji, ukeketaji na unyanyasaji.
Lyimo
alisema utaratibu wa BAWACHA kutoa tuzo kwa mwanamke jasiri utaendelea
kila mwaka ili kuionesha jamii kwamba mwanamke ni mtu muhimu katika
jamii na kwamba anao uwezo wa mkubwa kufanya kila jambo zuri la
maendeleo.
Naye
Akilimali aliwataka BAWACHA kufanya kazi kwa vitendo ili maendeleo
yaonekane kulingana na kaulimbiu ya dunia inayosema “ahadi ni ahadi
umefika wakati wa utekelezaji kivitendo, ukomeshaji wa ukatili dhidi ya
mwanamke na mtoto.”
Mwanaharakati
huyo mkongwe aliwataka wanawake kugombea katika nafasi za uongozi na
uamuzi ili kuuondoa mfumo dume na kuleta usawa wa kijinsia katika nyanja
zote za kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi.
Post a Comment