Ujumbe
umetumwa na mdau (nakushukuru) tokea mapema jana ila kwa bahati mbaya
ukatupwa kwenye kabrasha la mazagazaga kwenye anwani pepe, hadi
nilipoukuta humo wakati nakagua humo leo na kuutoa, nauwasilisha ulivyo:
AFIF, Saudi Arabia - Kijana mmoja nchini Saudi Arabia ambae alikua amehukumiwa kunyongwa baada ya kumwua mwanafunzi mwenzake mwaka 2008, hatimaye ameepuka kifo dakika za mwisho.
Baada ya kujaza fomu maalumu kwa ajili ya kujiweka tayari kupelekwa katika uwanja wa kunyongewa, Ahmad Matar AL-Qassami hakuamini masikio yake pale alipoambiwa kuwa familia ya marehemu, imekubali kupokea, “blood money”, Saudi Riyal milioni 5 (sawa na US$ 1, 666, 665).
AL-Qassami alihukumiwa kifo mwaka 2008 baada ya kumchoma mwanafunzi mwenzake na kumsababishia kifo. Alifikia hatua hiyo baada ya kutokea hali ya kutokuelewana kati yao wakiwa nje ya shule katika jimbo la Afif.
AL-Qassami aliambiwa na mnyongaji kuwa kuna msamaria mwema amejitolea kulipa adhabu hiyo ya blood money.
Baba mzazi wa AL-Qassami alisema alisujudu ili kumshukuru Mwenyez Mungu baada ya kuyanusuru maisha ya mwanaye.
Hili ni jambo la kawaida katika sheria za Saudi Arabia, kwamba kama umeua, ili unusurike na adhabu ya kunyongwa, basi familia ya marehemu inapaswa kukubali kupokea faini ya BLOOD MONEY, kama itakataa basi umekwenda na maji.

Post a Comment