DIAMOND APOTEZA TOUR YA EUROPE

Mwana muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, muite Diamond Platnumz,amezitosa shows mbili alizokuwa akafanye huko Europe. Diamond anaefanya vizuri kwenye muziki  na ndiyo star kwa sasa hapa Bongo,na anazidi kujipatia mashabiki wengi ikiwemo nje ya nchi ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook kwa mashabiki hao kuhusiana na show aliyokuwa akafanye huko.
Diamond akitoa sababu, alisema hatakuweko kama ilivyotangazwa mwezi huu na ni kwa sababu Kampuni/Promoter hao kushindwa kufikia mahitaji yaliyokuwa yakihitajika ikiwemo pesa pia.
Kupitia ukurasa huo, Diamond aliwaambia fans kuwa yeye na WASAFI hawatakuja kama ilivyotangazwa tarehe 15 mwezi huu na kwamba wasubiri mpaka atakaposema tena.

Post a Comment

Previous Post Next Post