Aliwahi
kuwa
katibu mwenezi wa klabu ya Simba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kondoa
kusini
Juma Selemani Nkamia amesema kujiuzulu kwa viongozi wa klabu ya Simba
ni pigo kwa klabu hiyo na kwamba kuna haja ya mwenyekiti wa klabu hiyo
kutafakari juu ya mustakabali wa klabu hiyo haraka iwezekanavyo.
Akiongea na
Rockersports Nkamia amesema habari za kujiweka pembeni kwa viongozi hao mjumbe wa kamati
ya utendaji ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo
Zakharia Hans Poppe na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geoffrey Nyange Kaburu zimemshitua sana na kwamba huenda kunasababu
iliyojificha nyuma ya pazia na kwamba kuna haja ya kuketi chini na kutafakari
kwa kina.
Amesema Has
Poppe amekuwa na mchangano mkubwa katika klabu ya Simba tangu wakati ule akiwa
ni kiongozi wa klabu hiyo na kwamba huenda kuna tatizo kubwa ambalo kiongozi huyo
ameliona na kuona bora akae pembeni jambo ambalo linatahitaji tafakari ya kina ya wanachama.
Nkamia
amesema
huenda tatizo likawa ni kwa mwenyekiti wa klabu hiyo kupingana na
maamuzi ya vikao halali vya wajumbe wa kamati ya utendaji au kujiamulia
mambo yake mwenyewe hali ambayo huenda ikapelekea wajumbe wengine
wakafuata nyayo hizo na kuleta athari kubwa kwa klabu hasa wakati huu
ligi ikiwa inaelekea ukingoni.
Amemuomba
mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaji Ismail Aden Rage kufanya busara kwa
kulitazama jambo hili kwa makini sana kwani huenda yeye akawa ndiyo
tatizo ndani ya klabu hiyo.
Post a Comment