KALA J’ HAJAWAHI KULIPIA VIDEO

Hiphop Artist anaetamba na single ya ‘Dear God’ kala Jeremiah amefunguka kuwa kichupa cha wimbo wake mpya #KaribuDar feat BenPol ambacho kimemulikwa na Dir AdamJuma wa visualLab ndio video ya kwanza ambayo msanii huyo ametoa pesa yake mfukoni kulipia.

KalaJ’ alifunguka hayo wakati alipokuwa akihojiwa kwenye kupitia kipindi cha FridayNightLive kinachorushwa moja kwa moja kwenye kituo cha televisheni cha Channel 5.
Msanii Kala Jeremiah ni miongoni mwa Star wakali wa muziki waliotokea kwenye shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search linalo ratibiwa na Kampuni ya Benchmark chini ya mkurugenzi wake Ritha Paulsen aka Madam Ritha.

Post a Comment

Previous Post Next Post