Moja viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar. |
KATIBU mkuu wa
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amesema kuwa michuano ya
Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar mwaka 2022 inaweza kuhamishwa
kutoka kipindi cha kiangazi na kuchezwa katika kipindi cha baridi kama
kutakuwa na ushahidi wa kitabibu ambao utaonyesha joto katika nchi hiyo
ya jangwa linaweza kuwaathiri wachezaji. Kauli
hiyo imekuja kufuatia rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA,
Michel Platini kutaka michuano hiyo ibadilishwe kutokana na joto kali
katika majira ya kiangazi ambalo hufikia hadi nyuzi joto 40. Akijibu
kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano
wa bodi ya kimataifa nchini Scotland, Valcke amesema suala la kuandaa
michuano ya Kombe la Dunia katika kipindi cha baridi linawezekana kama
kukiwepo ushahidi wa kitabibu kwamba haitawezekana kuchezwa katika
majira ya kiangazi kutokana na joto kali. Wanachosubiri
FIFA ni barua rasmi ya maombi kutoka Qatar ya kuhamisha michuano hiyo
katika kipindi cha baridi kama watakuwa wamemaliza uchunguzi wao na
kuona haitawezekana kwa wachezaji kucheza soka katika hali ya joto kali
katika majira ya kiangazi.
Post a Comment