
Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya imeamua kuwa rais
mteule Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto walichaguliwa
kwa njia huru na ya haki katika uchaguzi uliofanywa tarehe nne mwezi
Machi.
Umauzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika
mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada
ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.
Matokeo rasmi yalionesha kuwa Uhuru alishinda
uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata
asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya
uchaguzi kwa kura 8,100.
Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.
Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa
serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu
uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu
zaidi ya elfu moja.
Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William
Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia
za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.
Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha
ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha
uchaguzi mpya.
Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.
Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki
amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini
wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi
makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.
Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao
ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya
usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa
wapiga kura.
Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu
matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili
zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.
Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.
Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo
Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa
uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi
uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.
BBC
Post a Comment