Msemaji wa serikali ya Jamhuri
ya Afrika ya Kati, CAR, Gaston Makuzangba, ameiambia BBC kwamba mji
mkuu, Bangui, umejitayarisha kwa shambulio lolote la wapiganaji.
Hata hivyo kamanda wa wapiganaji, Arda Akouman, alisema Seleka wako kama kilomita 18 tu nje ya Bangui na wanataraji kufika mji mkuu usiku wa Jumamosi.
Aliwaomba watu wawe watulivu na jeshi liweke silaha chini.
Kuna taarifa piya za mapigano huko Boussambele, kilomita 160 kaskazini-magharibi ya Bangui.
Chazo:- http://www.bbc.co.uk
Post a Comment