Matukio baada ya mshindi kujulikana Kenya

Wafuasi wa Uhuru Kenyatta walijitokza mapema kusherehekea ushindi wa mgombea wao Uhuru Kenyatta katika eneo bunge la Gatundu
Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Hata hivyo tume ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano lakini kama inavyoonekana huenda tangazo hilo likachelewa
Popote ulipo kama mkenya au mwana Afrika Mashariki tupe maoni yako kuhusu yanayojiri pale ulipo wasiliana na si kupitia ukurasa wetu wa Bofya facebook na tutayaweka maoni hayo kwenye mtandao wetu Bofya bbcswahili.com

12:39 Lori lililokuwa limewabeba wafuasi wa Uhuru Kenyatta kutoka ngome yake ye Nyeri hususan eneo la Tetu, limeanguka, watu kumi wamejeruhiwa vibaya, mmoja amefariki na wengine zaidi ya 21 wanaendelea kupata matibabu

Wafuasi wa Uhuru Kenyatta
12:35 Maelfu ya wafuasi wa Kenyatta wakusanyika katika makao makuu yamuungano wa Jubilee, kumsubiri kiongozi wao wakati ukumbi wa Bomas ukiwa tayari kwa tangazo ya mshidni wa uchaguzi wa urais

11:32 Tume ya uchaguzi Kenya inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa kutangaza rasmi matokeo ya kura za urais

11:31 Mwandishi wa BBC Karen Allen kupitia twitter anasema moja ya kauli aliyoisikia leo ambayo imemfurahisha sana ni kumsikia mtu akisema kuwa wakenya ndio wameshinda uchaguzi kwa sababu wana taasisi mpya


09:51 Mjini Eldoret moja ya vitovu vya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007, leo ni uwanja wa sherehe za ushindi wa Uhuru Kenyatta. Bendera na kila aina ya mabango zinazobebwa na wafuasi wa Kenyatta ni ishara ya furaha yao. Eldoret pia ni ngome ya mgombea mwenza wa Kenyatta, William Ruto

09:23 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu ambayo ndio ngome kuu ya Raila Odinga, Ann Mawathe anasema kuwa wafuasi wa Odinga wamenuna kwa kuwa mgombea wao ameshindwa kwenye uchaguzi lakini wanaendelea na shughuli zao kama kawaida
08:45 Mjini Nyeri moja ya ngome za Uhuru Kenyatta ni vifijo na nderemeo tupu barabarani kusherehekea ushindi wake


08:12 Mjini Nakuru mamia ya watu waliamka asubuhi na mapema kusherehekea barabarani kafuatia taarifa za mgombea wao wa urais Uhuru Kenyatta. Wameonekana wakibeba mabango na matawi kama ishara ya furaha yao
08:06 Josiah Mayaka Wa Kisii Kenya anasema kupitia Bofya facebook kuwa watu wengi Kisii wamesononeka sana ila kwa sababu limetendeka wamekubali matokeo shingo upande.
07:47 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameimba wimbo wa taifa wakiwa kando ya majengo ya bunge kusherehekea ushindi wa mgombea wao


Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto
07:39 Mjini Eldoret ngome ya William Ruto mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta sherehe zimeanza mapema na asubuhi baada ya matokeo kudhihirika wazi kuwa Uhuru Kenyatta ndiye mshindi

07:35 Hanif Mohhamed wa Mombasa-Kenya kupitia ukurasa wa Bofya facebook naona mustakabali wa Kenya ni giza tupu, saa hii anasema anatafakari njia mubadala ya kukumbana na changa moto zitakazo wapata kama wakenya baada ya athari kuanza kuchimbuka.
07:26 Vifijo na nderemeo pamoja na milio ya honi katika barabara ya Kijabe mjini Nairobi kufuatia ushindi wa Uhuru Kenyatta

07:08Alex Mulwa kupitia ukurasa wa Bofya facebook anasema kuwa wakenya wamechagua viongozi ambao wataleta maendeleo na kuleta mabadiliko katika nchi yao. Alex ,kwa niaba ya wakenya anaomba ICC isitishe na kusimamisha kesi dhidi ya Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ili kuwapa nafasi kuongoza bila wasiwasi

06:55 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameanza kujitokeza katika baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi kusherehekea ushindi wake

06:46 Uhuru Kenyatta ana kura 6,173,433 wakati Raila Odinga 5,340,54. Hii inampa Uhuru ushindi wa asilimia hamsini nukta tatu ambao unahitajika chini ya katiba mpya kwa mtu kushinda uchaguzi wa rais.

06:40 Tume ya uchaguzi baadaye leo itatangaza mshindi wa uchaguzi ingawa hesabu ya kura inaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kinyang'anyiro. 
Chanzo:-  http://www.bbc.co.uk

Post a Comment

Previous Post Next Post