TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo Jumapili Machi 10, 2013
amemtembelea Mzee Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee wa Klabu ya Dar es salaam Young
Africans (YANGA), ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini
Dar es salaam, akiuguza majeraha kadhaa kufuatia kugongwa na pikipiki maarufu
kama 'Bodaboda' wiki iliyopita katika barabara ya Nyerere.
Rais Kikwete,
ambaye amewasili leo kutokea Afrika Kusini katika ziara ya kikazi ya siku
tatu, amempa Mzee Mzimba pole na
kumuombea apate nafuu ya haraka.
Katika ajali
hiyo Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha madogo usoni na
mikononi.
Kwa mujibu wa
madaktari na wauguzi hali yake inaendelea vyema baada ya kutibiwa, ikiwa ni
pamoja na kuvishwa Plaster of Paris (Piopio).
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
10
Machi, 2013

Post a Comment