Tanzania imepanda kwa nafasi nane katika viwango vya ubora
vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kutoka nafasi ya 127
waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 119. Wakati Tanzania ikiwa
nafasi ya 119 wapinzani wao katika kusaka tiketi ya kufuzu kwa Kombe la
Dunia 2014, Morocco wenyewe wanakamata nafasi ya 77, na Ivory Coast
(13) huku Gambia (144).
Mwezi uliopita pamoja na Taifa Stars kuichapa Cameroon 1-0, bado iliporomoka kwa nafasi tatu na kutoka 124 hadi 127. Nafasi ya juu zaidi iliyowahi kushika Tanzania kwenye viwango hivyo ni 65 mwaka 1996.

Post a Comment