Victoria Sound imezindulia katika ukumbi wa Mango Garden usiku wa tarehe
1.3.2013 . Saa sita na nusu usiku bendi hiyo ilipanda jukwaani na
kuanza kuwaonyesha wapenzi walio jazana Mango Garden kile ambacho bendi
imetayarisha. Hakika uingiaji wa bendi hii kwenye jukwaa ulikuwa wenye
ubunifu, ukanikumbusha uingiaji stejini kama huu wakati Muumin
alipoizindua Bwagamoyo Sound katika ukumbi wa Vatican Hotel Sinza miaka
kadhaa iliyopita. Mashabiki wa bendi hii ambao walijitayarisha kwa
mambango na sharashamra nyingi waliongeza uchangamfu katika uzinduzi
huu.
Kwa mara nyingine tena Waziri Sonyo alionekana jukwaani akiwa na ule
uimbaji wake wa sauti ya juu kuonyesha kuwa bado anakipaji cha uimbaji.
Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo Muumini atatakiwa ayazingatie ili
kujiweka sawa katika mpambano huu aliyojikita. Kwanza lazima kufanyia
kazi tatizo sugu la kukosekana kwa muziki ulio balanced, mafundi mitambo
wengi hudhani vyombo kulia kwa nguvu ndio kuonyesha ubora wa ufundi
wao, kinachotokea ni kelele ambazo hufanya kusikiliza muziki inakuwa
adhabu badala ya starehe. Pili ni lazima afanye tena mabadiliko katika
muziki wake kwani bado unafanana sana na bendi ambazo ziko hewani, hili
ni jambo la hatari kwani watu wanaweza kuona hakuna jipya kimuziki.
Wacheza show watalazimika kufanya mazoezi makali ili kujifua zaidi.
Post a Comment