Baadhi ya wapiganaji wa Kundi la waasi wa M23 wamekimbilia nchini Rwanda baada ya mapambano makali kati yao na waasi watiifu wa Sultan Makenga |
Na Martha Saranga Amini
Wapiganaji wa kundi la waasi wa M23 la nchini Jamuhuri ya kidemokrasia
ya Congo wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda baada ya mapigano makali
kati yao na wapinzani wao kutoka kundi la Sultan Makenga.
Waziri wa mambo ya kigeni nchini Rwanda Louise Mushikiwabo amethibitisha
kwamba takribani wapiganaji mia sita walikuwa miongoni mwa watu
waliovuka mpaka wa Rwanda na kuingia nchini humo siku ya ijumaa na
mapema jumamosi wakitokea eneo lenye machafuko nchini jamuhuri ya
kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zimebainisha kuwa wapiganaji hao waasi kutoka nchini DR Congo
wamenyang'anywa silaha na kuwekwa kizuizini huku baadhi wakitibiwa
majeraha na shirika la msalaba mwekundu.
Miongoni mwa wapiganaji hao alikuwepo kiongozi wa zamani wa kundi la m23
Jean-Marie Runiga, ambaye kikundi chake kimekuwa kikipigana na
wapinzani wake ambao ni askari watiifu wa kundi la kijeshi,linaloongozwa
na Sultani Makenga, tangu Machi 9.
Via kiswahili.rfi.fr
Post a Comment