Airtel Money yawakutanisha Wapiga picha wanahabari kwa semina ya siku mbili

Waandishi wa habari waliohudhuria semina ya ya upigaji picha  iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel jijini Dar Es Salaam.
Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingigwa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wapiga katika semina ya upigaji picha iliyofanyika jijini Dar Es Salaam, akifuatiwa ni Afisa uhusisano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki na Muhadhiri wa Chuo Kikuu Richard Ndunguru.
 *****     ******
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma yake ya kibebki ya  Airtel Money kwa mara ya pili imedhamini semina ya wapiga picha wanahabari inayofanyika kwa muda wa siku mbili hapa jijini Da r Es Salaam kuanzia leo 18 hadi 19 Apili 2012. 

Airtel kupitia  huduma yake ya Airtel Money imedhamini kampuni ya  jijini Dar es salaam ijulikanayo kama MP5 2011 entertainment kuandaa semina maalum itakayowakutanisha wataalam na wapiga picha za habari wa muda mrefu kukutana na wanahabari wapiga picha ili kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi za.

 Akiongea kwa niaba ya waandishi wapiga picha waliohudhuria semina hiyo Bw, Selemani Mpochi mpiga picha wa muda mrefu nchini alisema “hii ni sehemu muhimu sana kwetu wanahabari kujitengenezea utaratibu wakukaa pamoja na kutafakari mambo muhimu ili kuendelea kufanya kazi zetu kwa ufanis.

Kwa niaba ya wenzangu wote tunawashukuru sana Airtel kupitia huduma yao ya Airtel Money kwa kutudhamini katika semina hii kwa mara ya pili sasa, tunashukuru sana kwa ushirikiano wao wa kuwa tayari kutusaidia kuendeleza taaluma yetu na kuonyesha kuwa wanatambua umuhimu wa wanahabari ncin.i

Airtel inaendelea kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamenufaika kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi  kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hivyo semina hii ni njia nyingine itakayoweza kuinua kiwango cha mapato na uelewa wa Airtel Money kwa waandishi wa habari nchin.

Zaidi ya wapiga picha za habari wapatao 15 toka vyombo vya habari nchini wanatarajiwa kuhudhuria semina hiyo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa msimbazi center

Post a Comment

Previous Post Next Post