Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.
Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.
Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.
Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.
Katika mahojiano na jarida moja nchini Marekani mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Jarida hilo halikufanya mahojiani ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.
Wanawake wenye watoto ambao walihojiwa kwenye tafiti hizo walisema kwamba ajira zinawasumbua na wamefikiria kuwa ni ngumu kujigawa kazini na nyumbani kishughuli.
Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..
Wewe unaonaje toa maoni yako hapo chini
Post a Comment