
SIKU chache baada ya kuripotiwa akijiachia kimalavidavi na ‘lejendari’
wa Bongo Fleva, Aboubakar Katwila, staa wa muziki na filamu za Kibongo,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amenaswa hotelini na bwana Mzungu aliyetajwa
kwa jina moja la George, kamera za Risasi Mchanganyiko ni noma.
Shilole akiwa katika pozi na mzungu wake aitwaye George.
Kwa mujibu wa shushushu wetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika
hotelimoja maarufu jijini hapa ambapo Shilole alikuwa kwenye ziara ya
shoo yake.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo, Shilole
hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti
akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi
wa klabu moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.
...Wakiwa dukani.
Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato, Alhamisi
iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha
huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa
na maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na bwana huyo
ambapo Tulinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua kama ni wapenzi,
Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la kusema).
...Shilole na mzungu wake wakijiachia.
Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa
kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni
mambo ya kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani
shoo yangu ya Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana
Mwanza na siku moja nitaweka makazi hapa.”
...Wakikatiza mitaani
Post a Comment