| Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi akiwahutubia wananchi wa Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho uliofanyaka katika viwanja vya mpira Mkwajuni, April 06/2013 |
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema
Zanzibar ni nchi ya biashara hivyo inataka kujitegemea iweze kupunguza
ushuru ili wananchi wapate kununua bidhaa kwa bei nafuu.
Kauli hiyo ameitoa huko katika viwanja vya Skuli ya Mkwajuni Wilaya ya
kaskazini “A” wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa huo.
Amesema iwapo Zanzibar itapata mamlaka yake kamili itaweza kuwa na bandari huru, ushuru na bei za bidha vitapungua.
“Zanzibar ni nchi ya biashara tunataka tuwe na bandari huru ili tupate
kuweka kodi ndogo na ushuru ukipungua bei za bidhaa zitapungua”alieleza
Maalim.
Aidha amesema kuwa wananchi wanataka kuwepo kwa bandari na kupungua
ushuru ili wapate kuweka bei wanazotaka wenyewe na sio kuamuliwa na mtu
mwengine.
Akizungumzia Muungano Maalim Seif amesema wazanzibari waliowengi
wanataka serikali ya mkataba iwe na mamlaka kamili na isiingiliwe katika
maamuzi yake.
“Haya ni matakwa ya wananchi wenyewe na sio matakwa ya CUF hili ni la wazanzibar wenyewe” alieleza Katibu huyo.
“Zanzibar ni nchi matakwa ya wazanzibari yaheshimiwe yasiingiliwe na
wengine kwani mamlaka na madaraka hayo ndiyo yanayoweza kuyatatua
matatizo ya wazanzibar” alifafanua Maalim Seif.
Hata hivyo Katibu huyo ameitaka Tume ya kukusanya maoni ya Katiba
kuhakikisha kwamba wajumbe waliochaguliwa kuwakilisha kutoa maoni katika
Katiba hiyo wamechaguliwa kihalali na sio kupandikizwa.
Chanzo: zanzinews.com
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Post a Comment