
Diamond platinumz kila akitoa wimbo hushika attention ya watu wengi na
kuwa hit, lakini kumekuwa na mfululizo wa kesi za nyimbo zake kuvuja
ikiwa ni pamoja na wimbo wake wa ‘Ukimwona’ na video ya wimbo wake
‘Kesho’.
Hiki ndicho kilichotusababisha iwe na mashaka na kutoka kwa wimbo wake
mpya wa “Mapenzi basi” uliopikwa katika studio za AM Records, kutokana
na interval ya muda kwa kuzingatia kuwa bado ‘ Ukimwona’ haina muda
mrefu.
Tumemtafuta Diamond Platinumz ambae alifunguka kuwa wimbo huo ulivuja.
Aliwalaumu sana AM Records na kwa kile alichodai kuwa wanajua ni kwanini
wao wameamua kuvuja wimbo huo japo wanakwepakwepa.
“AM record wenyewe sijui wanachonitafuta ni nini nikirekodi nyimbo kwao wanakuwa wanazivujisha yani makusudi. ” Alifunguka Diamond. Alisisitiza kuwa anajua AM Records ndio wako responsible kwa zoezi la kuvujisha nyimbo zake, “yani ni wao mi najua kabisa ni wao, wanaongea ila wanakuwa kama wanakwepakwepa ila mi najua kabisa ni wao.”
Huu sio wimbo wa kwanza kwa Diamond platinumz kuwa na matatizo kutoka AM
Records, ‘Ukimwona’ pia ni wimbo ambao ulivuja na ulipikwa na AM
Records, lakini Nataka kulewa iliyozua gumzo pia ilifanyika katika
studio hiyo hiyo chini ya producer Maneck.
‘Kesho hit maker’ amesema baada ya wimbo wake ‘Ukimwona’ kupigwa sana
japo hakuitoa officially na imeshahit basi ameamua kuacha ipigwe tu
wakati anaangalia ngoma yake nyingine ya kuachia.
Tulinaendelea kufanya jitihada za kumtafuta Manecky wa AM Records ili
kujua kwa upande wake nini kinatokea hadi nyimbo za Diamond zinavuja
kutoka katika studio hiyo.
Sikiliza Interview yote hapa
Post a Comment