
Korea Kaskazini kuwaondowa wafanyakazi wake 53,000 katika eneo la viwanda la pamoja na Korea Kusini la Kaesong na kusitisha shughuli zote za kibishara katika kituo hicho kutokana na kile ilichokiita uchochezi wa kivita.
Kim Yang-Gon afisa mwandamizi wa chama tawala nchini Korea Kaskazini
amekaririwa akisema katika taarifa kwamba Korea Kaskazini itawaondowa
wafanyakzi wake wote katika kanda hiyo na wakati huo huo kusitisha kwa
muda shuguli zinazofanyika hapo na kuangalia iwapo iruhusu kuwepo kwa
kituo hicho au ikifungilie mbali.
Kim ambaye alitembelea kituo hicho cha viwanda cha Kaesong leo asubuhi
amesema wamelazimika kuchukuwa hatua hiyo kutokana na uchochezi wa
kivita unaotaka kuifanya Kaesong kuwa mahala pa malumbano kutokana na
kuongezeka kwa hali ya wasi wasi wa kijeshi katika Rasi ya
Korea.Ameongeza kusema kwamba hali itakavyokuwa huko mbele itategemea
mwenendo wa serikali ya Korea Kusini.
Wafanyakazi wa Korea Kusini wapigwa marufuku

Malori ya Korea Kusini yakirudi baada ya kuzuiliwa kuingia Kaesong.
Korea Kaskazini imewapiga marufuku mameneja wa Korea Kusini na
wafanyakazi wake kuvuka mpaka na kuingia katika kituo hicho cha viwanda
kilioko kilomita 10 ndani ya ardhi ya Korea Kaskazini tokea Jumatano.
Hadi sasa makampuni 13 kati ya 123 yenye kuendesha shughuli zake katika
eneo hilo yamelazimika kusitisha uzalishaji kutokana na uhaba wa mafuta
na mali ghafi. Zaidi ya wafanyakazi 300 wa Korea Kusini ambao walikuwa
wakifanya kazi katika kituo hicho cha viwanda cha Kaesong wakati
marufuku hiyo ilipotangazwa wamerudi Korea Kusini lakini zaidi ya 500
wameendelea kubakia katika kituo hicho.
Jaribio la nuklea haliko wazi
Wakati hayo yakijiri Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imekanusha dokezo
kwamba jaribio la silaha za nuklea linalotaka kufanywa na Korea
Kaskazini ni jambo lililo wazi na kwamba nyendo zilizorepotiwa kuwepo
kwenye mtambo wa nuklea wa nchi hiyo zilikuwa ni za kawaida.
Taarifa hii inapingana na kauli zilizotolewa awali na serikali ya nchi
hiyo.Tetesi zimekuwa zikiongezeka kwamba Korea Kaskazini itachukuwa
hatua fulani ya uchokozi hivi karibuni kwa kufanya jaribio la silaha za
nuklea au kufyetuwa kombora kufuatia wiki kadhaa za vitisho vya shari
dhidi ya Korea Kusini na Marekani.
Awali akizungumzia repoti za vyombo vya habari Waziri wa Korea Kusini
anayehusika na masuala ya muungano na Korea Kaskazini Ryoo Kihi-jae
ameiambia kamati ya bunge kwamba nyendo zilioko katika mtambo wao wa
nuklea zimeonyesha kwamba nchi hiyo inataka kufanya jaribio la silaha za
nuklea lakini alikataa kutowa ufafanuzi zaidi.
Ban aongezea sauti yake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametowa wito wa dharura
kwa Korea Kaskazini kujiepusha na uchokozi zaidi kufuatia repoti kwamba
inajiandaa kufyetuwa kombora jipya.
Ban amesema mjini The Hague Uholanzi kwamba Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Watu Korea haiwezi kuendelea kufanya namna inavyofanya kulumbana na
kupinga mamlaka ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya
Kimataifa kwa jumla.
Akizungunmza na waandishi wa habari Ban amesema hilo ni "ombi la dharura
na la uadilifu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na kutoka kwake
binafsi."
Post a Comment